
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa Msjid Fatma
kwa Muhammed Ali Kidongochekundu Wilaya ya Mjini Unguja, alipowasili kwa ajili
ya Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika leo 18-10-2024 katika msikiti huo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Waumini wa
Dini ya Kiislamu baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika
katika Masjid Fatma kwa Muhammed Ali Kidongochekundu Wilaya ya Mjini Unguja leo
18-10-2024
WAUMINI wa Dini ya Kiislamu wakimsikiliza Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi
(hayupo pichani) akizungumza na kuwasalimia baada ya kumalizika kwa Ibada ya
Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid Fatma kwa Muhammed Ali
Kidongochekundu Wilaya ya Mjini Unguja leo 18-10-2024
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsalimia Ndg. Salum Othman, baada ya
kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid Fatma kwa
Muhammed Ali Kidongochekundu Wilaya ya Mjini Unguja leo 18-10-2024RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsalimia Ndg. Salum Omar Khamis,
baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid
Fatma kwa Muhammed Ali Kidongochekundu Wilaya ya Mjini Unguja leo 18-10-2024
RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al hajj Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewanasihi Waumini wa dini ya Kiislamu kujitathmini na kujua
umuhimu wa Ibada kwenye matendo yao ya kila siku.
Alhaj Dk. Mwinyi ametoa nasaha hizo leo tarehe 18 Oktoba 2024
alipotoa salamu kwa Waumini hao baada kujumuika nao kwenye ibada ya sala ya Ijumaa, msikiti wa
Muhammad Ali, Kidongo Chekundu, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Ameeleza, ni wajibu wa kila Muumini kuitathmini nafsi yake na
anaowaongoza ili kubaini kiasi gani maisha yao yanalingana na Ibada wanazozitekeleza
kila siku.
Amesema, kuna mambo mengi yanaendelea ndani ya jamii kwa sababu
ya watu kukosa Ucha Mungu(taqwa).
Pia Alhajj Dk. Mwinyi ametaja baadhi ya mambo hayo kuwa ni
pamoja na Udhalilishaji, ubakaji na Wizi.
Aidha, amewahimiza Waumini hao kufanya Ibada kwani Ndio sababu
kuu ya kuumbwa kwao.
Akitoa Salamu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Muft wa Zanzibar,
Sheikh Khalid Ali Mfaume amewasisitiza viongozi kuwa mfano bora kwa watu
wanaowaongoza kwa kutenda mambo mema.
Amewasisitiza Vijana kuacha kushawishika na kujiunga na
makundi maovu kwa kisingizio cha dini badala yake kusimamisha sala kwa
kuchunga wakati na nidhamu.
IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment