Habari za Punde

BARAZA LA MAPINDUZI KUANGALIA SERA MPYA YA MAGEUZI YA UTALII

Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, akiongoza kikao kazi cha kupitia sera ya mageuzi ya  kimkakati katika  sekta ya Utalii, kilichowashirikisha makatibu wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kufanyika hoteli ya  Golden Tulip UIwanja wa Ndege. (PICHA NA FAUZIA MUSSA)

Na Rahma Khamis  Maelezo   8/12/2024

Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said amesema upitishwaji wa sera mpya ya mageuzi ya  Utalii  mwaka 2024 itasaidia kuondoa changammoto zilizokuwepo hapo awali.

 Ameyasema hayo katika Ukumbi wa Golden Tulip UIwanja wa Ndege wakati akifungua kikao KAZI Cha kupitia sera ya mageuzi ya  Kimkakati katika  Sekta ya Utalii uliyowashirikisha Makatibu Wakuu Serikali ya Mapinduzi ya zanzibar.

Amesema kuwa ili Sekta ya  Utalii ibadilike Wizara lazima ishirikiane na Wadau mbalimbali wa Utalii ili kukuza Sekta hiyo na kuleta mabadiliko

Amesema baada ya kupitisha sera hiyo itapelekwa Baraza la Mapinduzi wa kuangaliwa zaidi kabla ya kuanza kutumika ili iweze kukidhi haja. Utalii wa kielimu kwa kuanzisha vyuo vya kutoa elimu kuhusiana na Utalii ili kuongeza Pato la Taifa

Aidha amefahamisha kuwa   Wizara imefanya KAZI kubwa ya kuichambua sera iliyopo awali na  kuangalia mapungufu na changammoto zilizomo ili kurekebisha changammoto hizo.

Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale  Abuod Suleiman Jumbe amesema kuwa maono ya Dkt Hussein  Mwinyi katika kuhakikisha sekta ya Utalii inakua  juhudi mbalimbali zimefanyika ikiwemo kushirikiana na Wadau mbalimbali wa Utalii lengo ni kuleta mageuzi katika sekta hiyo pamoja na urithi wa mambo ya Kale

Amesema kuwa ndani ya miaka minne kumekua na mabadiliko ya haraka katika Utalii na urithi wa mambo ya Kale .

Ameeleza kuwa wabaini kuwa sera hiyo imeshapitwa na wakati na kupitishwa sera mpya ambayo inatoa  vipaumbele kwa wananchi.

"Sera hii inakwenda sambamba zaidi vivutio vya Utalii na Utalii w Michezo wa mpira wamiguu kwa kuzingatia maslahi ya wananchi wote, alisema Katibu.

Aidha amefahamisha kuwa sera hiyo ni sera ambayo imeweka waziri na kuzingatia vipaumbele kwani ifikapo 2025 kuingiza watalii l mlioni moja kwa mwaka

Aidha amefahamisha kutokana na mageuzi hayo ya  kimkakati imepelekea kuifungua Pemba kitalii na kujitokeza kwa wadau mbalimbali  kuunga mkono juhudi za hizo.

Nao Wadau wa Utalii  wamesema sera hiyo itahakikisha inazingatia mazingira ya wazanzinar  ili kua  endelevu .

Kwa upande wake  Mkurugenzi wa Wizara hiyo  Abdalla Muhammed Juma ameeleza kuwa sera hiyo ya mwaka 2017 imepitwa  hivyo  ipo haja ya kubadilisha kwani Kuna mambo muhimumu yamenitokeza ikiwemo ushirikishwaji wa wananchi katika Utalii pamoja na bidhaa za kitalii

Aidha amesema ushirikishwaji wa Sekta nyengine za binafsi utasaidia kuwapa uwelewa  zaidi Kufahamu dhana ya Utalii kwani unaenda sambamba na mipango na mikakati  ya kulinda Utamaduni wa Mzanzibar .

 Nao Washiriki wa kikao hicho wamesema kuwa sera hiyo ni vyema itoe kipaombele kwa  wananchi kwani il Utalii uzidi Kukuwa kwa kuzingatia mazingira

Kikao hicho kimeandaliwa na Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale kwa kushirikiana na  Tony Blair Insitute for Global chang.


MAELEZO PICHA.

Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, akiongoza kikao kazi cha kupitia sera ya mageuzi ya  kimkakati katika  sekta ya Utalii, kilichowashirikisha makatibu wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kufanyika hoteli ya  Golden Tulip UIwanja wa Ndege. (PICHA NA FAUZIA MUSSA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.