Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman akiondoa pazia kuweka Jiwe la Msingi la ufunguzi wa Mradi wa Utalii Rafiki na Mazingira katika Msitu wa Masingini Wilaya ya Magharib "A" Unguja, ikiwa ni Shamrashamra za Miaka 61 ya Mapinduzi Matukifu ya Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanziar Mhe. Othman Masoud Othman, amesema kwamba ni muhimu kuendeleza jitihada za kuwawezesha wananchi kiuchumi ili waweze kuzitumia ipasavyo fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta ya utalii na kuchangia kukuza uchumi na maendeleo ya nchi.
Mhe. Othman ameyasema hayo huko Msitu wa Masingini Wilaya ya Magharib "A" Unguja alipoweka jiwe la msingi la Mradi wa
Utalii Rafiki na Mazingira, unaomilikiwa
na Kampuni ya Zanzi Eco- Tourism wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia
tisa ikiwa ni shamra shamra za kuelea maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar ya mwaka 1964 .
Amefahamisha kwamba Zanzibar
kupitia rasilimali za asili kama vile misitu upo uwezekano mkubwa wa wananchi
kuwekeza na kuweza kupata faida na kwamba kampuni iliyoanza kuwekeza kwenye
msitu wa masingini imeonesha njia.
Hivyo Mhe. Othman amesisitiza
kwamba suala la hifadhi ya mazingira ni muhimu kwa maisha ya wanadamu na kwamba
Kampuni hiyo ni vyema kupanua wigo wake na kuwekeza sehemu nyengine katika
visiwa vya Unguja na Pemba.
Amezitaka wizara za kilimo na Mamalaka
zinazohusika na uwekezaji kutafuta wawekezaji wengine zaidi kuwekeza katika
miradi rafiki na mazingira kwenye misitu tofauti ya hifadhi iliyopo katika visiwa vya Unuja na Pemba
kwani kufanya hivyo kutaweza kuleta tija zaidi kiuchumi kupitia maliasili hiyo
.
Hata hivyo, Mhe. Othman amesitiza
haja ya Mamlaka zinazousika na hifadhi ya Misitu kuendelea kuilinda msitu huo wa Masingini kwa
kuwa ni chanzo kikubwa cha upatikanaji wa Maji katika maeneo mbali mbali
ukiwemo mji wa Zanzibar na pia upatikanaji wa hewa safi na salama kwa uhai wa
wanadamu.
Hatua hiyo amesema
itasaidia katika kuhakikisha misitu na rasilimali zake inakuwa endelevu
na kwamba ni muhimu kwa wananci kujenga tabia
ya kulinda na kihifadhi misitu ili matunda yake yaendelee
kunufaisha sasa na vizazi vijavyo.
Amesema kwamba Zanzibar ikilelea na
uwekezaji wa miradi ya aina hii ni wazi
kwamba itachangia sana kutatua changamoto za kimazingira ikiwemo uvamizi holela
wa Misitu pamoja na ukataji wa miti.
Kwa upande wake Waziri wa Kilimo ,
Umwagiliaji,Maliasili na Mifugo Shamata Shaame Khamis amesema kwamba mradi huo
awamu ya kwanza utasaidia kukamili
changamoto ya uharibifu wa Mazingira kwa kurejesha shukrani kwa wananchi kwa
kuwapa gaiwio la faida linalotokana na uwekezaji huo.
Aidha amesema pia mradi huo unaibua
fursa zaidi ya kuongeza vivutio vya na fursa zaidi za utalii ili kufikia
matumaini ya taifa katika suala la kukuza ajira kwa wananchi.
Naye mmiliki wa Mradi huo Alan
Peter Nnko, amesema kwamba mbali na hifadhi ya mazingira mradi huo utakuwa na
faida kubwa kwa wanawake kusaidia ajira na kueleza kwamba awamu ya kwanza ya
maradi huo, utakaokuwa na daraja la kuangalia msitu, mkahawa, nyumba ya juu
ya miti , daraja la kunesanesa na
vivutio vyengine na hadi sasa ushagharimu zaidi ya shilingi milioni mia tisa.
Mwishwo
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Kitengo chake cha habari leo Jumapili Disemba 28 mwaka 2024.
No comments:
Post a Comment