Habari za Punde

Wataendelea Kuwapa Mafunzo Vijana ili Waweze Kuzifikia Fursa Mbalimbali

Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita akikabidhi fedha taslim Sh. Milioni mbili na laki 5, huko Ofisini kwake Migombani, ikiwa ni ahadi walioiweka na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mhe. Sharif Ali Sharif katika Tamasha la Samia Fation Fastival 2024 ambalo liliofanyika Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa ndege hapo juzi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mhe. Sharif Ali Sharif ameshiriki katika makabidhiano ya fedha taslim Sh. Milioni mbili na laki 5, ikiwa ni ahadi walioiweka kwa kushirikiana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita, katika Tamasha la Samia Fation Fastival, liliofanyika Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa ndege hapo juzi.

Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita amesema wataendelea kuwapa mafunzo Vijana ili waweze kuzifikia fursa mbalimbali zilizopo ikiwemo Mikopo.

Ameyasema hayo huko Ofisini kwake Migombani mara baada ya kukabidhi fedha taslim kwa Vijana waliopata nafasi 5 bora katika Tamasha la Samia Fation Fastival 2024, lilifanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa ndege hapo juzi.


Amesema kuna vijana wanakosa imani na Serikali, wakidhani hawapewi jambo ambalo linawakatisha tamaa lakini jambo kubwa linalopelekea kuzikosa ni kushindwa kuzipambanua fursa hizo.


Aidha amesema Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kushirikiana na Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji itahakikisha Vijana hao wanapata fursa za kuwezeshwa ili waweze kuanzisha Miradi ya Maendeleo.


Hata hivyo amewataka Vijana kujuwa namna ya kuzitumia fedha hizo wakati watakapopatiwa fedha ikiwepo ikiwemo Mikopo ili kuwawezesha na wengine kupata fursa hizo.


Nae Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mhe. Sharif Ali Sharif amewataka wanamitindo hao kuvaa nguo za Stara zinazoendana na maadili ya kizanzibar.


Mbali na hayo Mhe. Sharif amewataka kuisaidia Serikali katika kuielimisha jamii juu ya suala la mavazi ya stara kwa lengo la kulinda Tamaduni za Mzanzibar.


kwa upande wake Muandaaji na Muanzilishi wa Tamasha la Samia Fation Fastival bi Khadija Mwanamboka amewaahidi kuwasimamia Vijana hao ili waweze kuendelea mbele na kuwa mabalozi wazuri kwa wenzao.


Vijana 5 waliokabidhiwa fedha taslim na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita kwa kushirikiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mhe. Sharif Ali Sharif ni pamoja na Khadija Abdulfatah, Thurea Khamis Said Design, Said Ali Hassan, Shomari Makame Waziri na Zanzibar suti ambapo kila mmoja amekabidhiwa Fedha taslim Sh. Laki 5.


Imetolewa na Kitengo Cha Habari, Mawasikiano na Uhusiano, 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.