Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Amuwakilisha Rais wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika Kuhusu Kilimo

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini mbele ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda  (kushoto) na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika baada ya kushuhudia  Tamasha la Kahawa Afrika. Africa Coffee Festival)  lililolenga kuhamasisha   uongezaji  thahamani katika mazao yanayolimwa Afrika likiwemo zao la kahawa. Tukio hilo lilifanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Speke Resort, Munyonyo, Kampala Uganda ambako alimwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika Mkutano Maalum wa  Wakuu wa Nchi na  Serikali wa Umoja wa  Afrika kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Afrika, Januari 11, 2025. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na baadhi ya Wakuu wa Nchi  na Serikali wa Umoja wa  Afrika wakisikiliza wimbo wa taifa wa Uganda katika ufunguzi wa Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika  kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Afrika uliofanyika  kwenye Kituo cha Mikutano cha  Speke Resort Munyonyo, Kampala Uganda, Januari 11, 2025. Waziri Mkuu alimwakilisha Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wenye mkutano huo.
 Rais Yoweri Museveni wa Uganda  (wa nne kushoto) pamoja na viongozi wengene wakifuatilia hotuba ya Waziri Kassim Majaliwa aliyoitoa wakati alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha  Speke Resort Munyonyo, Kampala Uganda,Januari 11, 2025.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha  Speke Resort Munyonyo, Kampala Uganda, Januari 11, 2025.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Jakaya Kikwete wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika baada ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda kufungua Mkutano Maalum wa  Wakuu wa Nchi  na Serikali wa Umoja wa  Afrika kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Speke Resort Munyonyo, Kampala Uganda, Januari 11, 2025.  Waziri Mkuu alimwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Kwenye mkutano huo.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.