Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fatma Hamad Rajab, amesema Serikali inafanya juhudi mbali mbali kuhakikisha vijana wanapata nyenzo za kujiari wenyewe kupitia mafunzo ya amali.
Akizungumza na ugeni kutoka chuo cha Veta uliokuja Zanzibar kwa lengo la kubadilishana uzoefu kwa vijana kwenda kujifunza mafunzo ya amali, amesema hatua hiyo itasaidia kuwa na wataalamu katika sekta mbali mbali pamoja na kuongezeka kwa fursa za ajira.
Aidha amesema Serikali inachukuwa juhudi mbalimbali kuhakikisha Vijana wanapata nyenzo kujiajiri wenyewe kupitia mafunzo ya amalina kupata ajira ili waweze kuachana na Vitendo Viovu ikiwemo utumiaji wa Dawa za kulevya,Bangi na Dawa za kulevya.
Hata hivyo ameupongeza Ugeni huo kwa mashirikiano makubwa wanayoyaonyesha kwa Wizara ya habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na kuamua kujitolea kuja Zanzibar kwa ajili ya kuonyesha fursa mbalilmbali zinazoweza kupatikana kupitia vyuo vya Veta.
Mkurugenzi wa Veta kanda ya mashariki, nd. John Mwanja amesema wameota Zanzibar kuna vijana wengi wenye ujuzi lakini hawana vyeti vya uthibitisho hivyo amesema wanampango maalum wa kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa Vijana wa Zanzibar hasa katika Mahoteli ili vijana hao waweze kuwapatia vyeti na kuweza kutambulika.
'' Sisi umeandaa mpango maalum wa kuwafata vijana walipo na kutoa mafunzo ya muda mfupi kwani ni vigumu kumtoa kijana ambae tayari ameshakuwa na majukumu kumpeleka Tanzania Morogoro, Mwanza au maeneo mengine, kujifunza kwa muda wa miaka minne wakati tayari ameshakuwa na majukumu ya familia''alisema Mkurugenzi Mwanja.
Aidha amesema ujio huo ni kuonesha fursa zilizopo katika chuo cha Veta na kuzileta kwa vijana wa Zanzibar wenye ujuzi ambao hawajapata mafunzo ya Veta ili kuisaidia Serikali katika kuwapatia vijana ajiara ikiwa ni kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi mwaka 2020-2025.
kwa uapande wake Mkuu wa chuo cha Veta Mkoa wa Morogoro nd. Salum Ulimwengu amesema wanatoa mafunzo mbalimbali ikiwemo ya Hoteli na usafirishaji wa magari makubwa yanaakisi uwepo wa miundo mbinu bora katika visiwa vya Zanzibar.
Ujumbe huo pia umefanya ziara katika maeneo mbali mbali ikiwemo kituo cha mafunzo ya vijana Bweleo , uwanja wa Amani Complex na kumalizia katika viwanja vya michezo Maisara pamoja na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu CCM, Nd. Mohammed Said Dimwa .
Imetolewa na kitengo cha habari, mawasiliano na uhusiano,
WHVUM.
No comments:
Post a Comment