Habari za Punde

ZOEZI LA UANDIKISHAJI LAENDELEA MAGHARIBI B UNGUJA

 

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jaji Aziza Idi Suwedi (kulia)akimsikiliza  Mkuu wa Kituo cha Uwandikishaji Wapiga Kura Shehia ya Shakani Makame Talib Makame walipofanya Ziara Maalum ya Kutembelea Vituo mbalimbali vya Uandikishaji na kutatua Changamoto Zilizojitokeza katika Wilaya ya Magharibi B Unguja.

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jaji Aziza Idi Suwedi akiwa pamoja na Makamishna wa Tume hio wakitoka kukitembelea moja kati ya Vituo vya Uwandikishaji Wapiga Kura katika Ziara Maalum ya Kutembelea Vituo mbalimbali vya Uandikishaji na kutatua Changamoto Zilizojitokeza katika Wilaya ya Magharibi B Unguja.
Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Juma Haji Ussi akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kumaliza kwa  ziara  Maalum ya Kutembelea Vituo mbalimbali vya Uandikishaji na kutatua Changamoto Zilizojitokeza katika Wilaya ya Magharibi B Unguja.

PICHA NA YUSSUF SIMAI,MAELEZO ZANZIBAR.05-03-2025

Na Rahma Khamis Maelezo               6/3/2025

Kamishna Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC Juma Haji Ussi amewataka wakaazi wa Wilaya ya Kati kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura linalotarajiwa kuanza Mach 8


Wito huo ameutoa Skuli ya Fumba Wilaya ya Magharibi B' wakati akitembelea vituo vya kuandikisha daftari la wapiga  kura ikiwa ni muendelezo wa ziara ya  kukagua vituo hivyo

 

Amesema kwa mujibu wa taarifa wanazozipata kupitia vituo hivyo zoezi linafanyika kwa amani na utulivu hakuna tatizo lolote na kila mwananchi mwenye sifa ya kuandikishwa kwenye daftari hilo la wapiga kura amepata haki yake ikiwa ni maandalizi ya kupiga kura 

 

Wakuu wa Vituo vya uandikisha daftari hilo wamesema kuwa zoezi linaendelea vizuri changamoto zilizopo ni ndogo ndogo kwenye mashine za kusomea vidole ambazo wameweza kuzitatua na kuendelea kufanya kazi.

 

Nao wananchi waliofika kuandikishwa katika daftari hilo wamesema kuwa kujiandikisha ni haki ya msingi kwani unaweza kufanya maamuzi sahihi wakati wa uchaguzi bila ya kubugudhiwa .

 

Aidha wamewaomba wananchi wenzao ambao bado hawajajiandikisha katika daftari la wapiga kura kujitokeza ili kupata nafasi ya kupiga kura unapofika uchaguzi.

 

Katika ziara hiyo vituo mbalimbali vilitembelewa ikiwemo Fumba, Nyamazi, Maungani Kisauni Bweleo na Dimani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.