
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, ameanza ziara ya kikazi katika Mkoa wa Mara kuanzia tarehe 22 hadi 25 Aprili 2025. Ziara hii inalenga kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025, kuimarisha uhai wa chama, pamoja na kusikiliza kero za wananchi na wanachama wa CCM.
Katika ziara hiyo, Dk. Nchimbi atatembelea wilaya mbalimbali zikiwemo Bunda, Musoma, Butiama, Rorya, Tarime Mjini, Tarime Vijijini, na Serengeti. Akiwa katika maeneo hayo, atakagua miradi ya maendeleo, kuzungumza na wananchi, na kutoa maelekezo kwa viongozi wa chama na serikali juu ya utekelezaji wa majukumu yao kwa ufanisi zaidi.
Ziara hii ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, ambapo CCM inalenga kuendelea kutekeleza Ilani yake kwa ufanisi na kwa kuzingatia mahitaji halisi ya wananchi.
No comments:
Post a Comment