Na Miza
Chande-Maelezo Zanzibar
Waziri wa Nchi
Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mohammed Aboud Mohammed ameuhakikishia
umoja wa Mapadri nchini kuwa malalamiko ambayo wameyatoa kwa Serikali atayawasilisha
kwa maandiko kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Kikwete na
Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohammed Shein.
Malalamiko hayo
yanatokana na vurugu ambazo zilitokea mwishoni mwa wiki katika maeneo ya mji wa
Zanzibar ambapo Makanisa matatu yalichomwa moto
na kusababisha uharibifu wa mali
mbali mbali za Makanisa.
Waziri Aboud
ameyasema hayo alipokutana na Ujumbe wa umoja wa Makanisa Tanzania ulioongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa
Anglikana Dk. Valontine Mokiwa katika Afisi ya Waziri huyo Mjini Zanzibar .
Amesema Serikali
na kila mwananchi mpenda amani amehuzunishwa sana na fujo zilizotokea na kuahidi kuwa
Jeshi la Polisi linaendelea kufanya kazi yake ya kuwatafuta wale wote
waliohusika na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Waziri Aboud amesema
amefurahishwa na subra ambayo Wakristo hao wameichukua bila ya kulipiza kisasi
jambo ambalo linawajengea heshima kubwa kwa jamii.
Amezisisitiza
Taasisi za dini kuendelea kuhubiri amani kama lengo la taasisi hizo linavyosema
na kuongeza kuwa kama kuna mambo ambayo
yanafaa kuzungumzwa ni suala la ukosefu wa ajira na umasikini nchini.
Amesema Viongozi
wa Dini wanapaswa kuwa na mipaka,busara na elimu wa yale wanayoyahubiri na
kuwataka wananchi kuweza kuchambua juu ya viongozi ambao wanafaa kusikilizwa na
wale ambao hawafai kusikilizwa.
Aidha
amewahakikishia Viongozi hao wa dini kuwa na amani na kwamba ulinzi
umeimarishwa katika Sehemu zao za ibada ili kuweza kuzuia watu ambao hawaitakii
mema Zanzibar .
Kwa upande wake
Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Dk. Valontine Mokiwa amesema kuwa matukio
ambayo yamekuwa yakifanyika yamepindukia mpaka Zanzibar lakini Serikali ya
Mapinduzi imekuwa imeonekana kuwa na imani kubwa wakati hali inakuwa mbaya.
Amdai kuwa Makanisa
25 katika Visiwa vya Unguja na Pemba tokea
mwaka 2001 yameshambuliwa lakini hakuna hatua yoyote ambayo imechukuliwa kwa wahalifu
hao jambo ambalo linawapa shaka.
Mokiwa amesema
Jamii ya Wakristo nchini ina hamu ya kujua nani kahusika na kuchukuliwa hatua
za kisheria na siyo tu kuishia kuambiwa Jeshi la Polisi linaendelea kuwatafuta
wahalifu hao.
0 Comments