Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KOCHA wa Riadha wa timu ya Tanzania inayotarajiwa kushiriki mashindano ya
Olimpiki London, Zakaria Gwandu, ameelezea kusikitishwa na kushangazwa kwa
mchezaji Faustine Mussa kutojiunga na wenzake kambini, Mkuza Kibaha.
Mashindano hayo ya Olimpiki yanatarajiwa kufanyika jijini London, Uingereza
kuanzia Julai 27 hadi Agosti 12 mwaka huu.
Kocha huyo amekaririwa jana akisema kuwao, wakati timu ikitarajiwa kuondoka
nchini Julai 8 mwaka huu, Mussa ambaye ni mwajiriwa wa Jeshi la Wananchi Tanzania,
ndiye pekee ambaye hajajiunga na kambi hadi sasa, jambo alilosema linamuweka
katika wakati mgumu kutekeleza programu zake.
“Ninachoweza kusema ni kwamba sifahamu kinachoendelea kuhusiana na mchezaji
Faustine Mussa, sijui tatizo ni kwa mchezaji au mwajiriwa wake, kwani Chama cha
Riadha kilikwishatuma barua ya kumuombea ruhusa mwajiri wake muda mrefu, lakini
bado hajaonekana kambini,” alieleza kwa huzuni kocha huyo.
Timu ya riadha itakayoshiriki michezo ya Olimpiki nchini Uingereza, inaundwa na
wachezaji wanne, ambao ni Zakia Mrisho, Samson Ramadhani, Msenduki Mohamed na
Faustine Mussa, ambaye bado hajaripoti kambini.
WAZIRI MKUU AKUTANA NA BALOZI WA JAPAN NCHINI
-
WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amekutana na Balozi wa Japan nchini
Tanzania Mhe. Yoichi Mikami na kujadiliana naye masuala ya uchumi, miradi
ya maendel...
0 Comments