6/recent/ticker-posts

Ligi kuu Zenj yafikia nusu njia

Na Mwajuma Juma
 
Mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya soka Zanzibar ‘Grand Malt’, unatarajiwa kufikia tamati leo kwa mechi moja itakayozikutanisha timu za Mafunzo na Mtende Rangers katika uwanja wa Amaan.
 
Matokeo ya pambano hilo ndiyo yatakayotoa picha halisi ya timu gani itashika hatamu za ligi hiyo ambapo kwa sasa inashikiliwa na KMKM yenye pointi 23.


Aidha, kukamilika kwa mzunguko huo, kunatoa nafasi kwa klabu zinazoshiriki ligi hiyo kufanya usajili wa dirisha dogo kuanza mapungufu waliyoyabaini katika vikosi vyao.
 
Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), kimepanga usajili huo uanze Disemba 15 hadi Januari 15, mwaka huu.
 
Iwapo Mafunzo yenye pointi 24 itashinda leo, itafikisha pointi 24 na kuwaengua kileleni mabaharia wa KMKM.
 
Mzunguko wa pili wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 12 za Unguja na Pemba, unatarajiwa kuanza mwezi Februari mwaka 2013.
 
Wakati huo huo, katika mechi ya ligi hiyo iliyochezwa juzi uwanja wa Amaan, timu za Mundu na Chipukizi zilishindwa kutambiana na kutoka sare isiyo na magoli.

Post a Comment

0 Comments