Na
Haji Nassor, Pemba
MAKAMU
Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, amesema serikali
haitomvumilia mtu ama kundi lolote, litakalotumia dini kuwachonganisha
wananchi.
Aliyasema
hayo jana, katika uwanja wa mpira Makombeni, baada ya kufungua tawi la kisasa
la CCM Makombeni, na kisha kuzungumza na wanaCCM na wananchi kwenye mkutano wa
hadhara.
Alisema,
katika siku za hivi karibuni, kumeibuka makundi yanayotumia vibaya fursa ya
kutangaaza dini na kuchukua baadhi ya vipengele vya siasa kwa lengo la kuwababaisha
wananchi, jambo ambalo halileti taswira nzuri kwa taifa la kistaarabu na
lililotawaliwa na amani kama Zanzibar.
Alisema
wale wote wenye tabia hiyo mbaya, kamwe serikali kwa kushirikiana na vyombo
vyake, haitowavumulia kwani wamekuwa wakiitumia fursa hiyo vibaya.
Alisema
huu si wakati tena wa kuirudisha Zanzibar iliko toka na badala yake fursa za
kujikusanya pamoja zitumiwe kuhubiri umoja na mshikamano.
“Iwe
kundi lolote, la Mlalo, Uamsho au watu wengine, kama wakitumia vibaya fursa ya
kutangaaza dini, na kujificha kwenye mambo ya kisiasa kwa lengo la kuwagawa wananchi,
nasema hawatovumiliwa,’’alionya Dk. Shein.
Dk.
Shein ambae ni Rais wa Zanzibar alisema serikali tayari imeanza mchakato wa
kuifanya hospitali ya Abdallah Mzee ya Mkoani, kuwa ya mkoa kama alivyoahidi wakati
wa kampeni.
“Wakati
tulipokuwa tukipita kuomba ridhaa ya kuingia ikulu, tulisema mkituchagua
tutafanya mengi, ikiwa ni pamoja na kuifanya hospitali hiyo kuwa ya mkoa, sasa
mambo yameanza taratibu,” alisema.
Kuhusu
dhana zilizoibuka hivi karibuni, kwamba vyama vya upinzani vitamuondoa Dk.
Shein madarakani, kutokana na wingi wa kumiliki vitambulisho vya Mzanzibari,
alisema wamechelewa.
Alisema
yeye hawezi kung’olewa madarakani kwa wingi wa vitambulisho hivyo
vinavyomilikiwa na wafuasi wa chama fulani, kwani kinachohesabiwa siku ya
uchaguzi mkuu ni kura na sio vitambulisho.
Dk.
Shein alisema wenye ndoto hizo wamechelewa na wamekuwa wakiota ndoto za mchana,
ambazo hukosa jawabu makini na kubaki wakitapatapa.
Kuhusu
katiba ya Zanzibar, alisema kila mmoja anawajibu wa kuifuata kwa vitendo, kwa sababu
hakuna mtu wala kundi la watu lililojuu
ya katiba ya nchi.
Katika
hatua nyengine, Makamu Mwenyekiti huyo wa CCM Zanzibar, aliwataka vijana,
waache tabia ya kukimbilia nje ya nchi kwa kutafuta kazi, na badala yake
watulie nchini ili kujikusanya pamoja kwenye vikundi vya ushirika.
Alisema
serikali imekuwa mbioni kila siku kuhakikisha vijana wake wanawezeshwa kupitia
vikundi vya ushirika, kwani haina uwezo wa kuajiri kila mmoja.
“Vijana
wangu acheni kumilikiwa kiakili, kwamba leo mtapelekwa Qatar, kesho Marekani,
baadae Afrika Kusini, jamani bakini nyumbani
mkiwa na malengo yenu, na serikali yenu inawahangaikia,’’alisema.
Mapema
aliwakabidhi kadi za CCM wanachama wapya 291wakiwemo wa Jumuia za CCM.
Awali
Dk. Shein alitembelea tawi la CCM la Mizingani na kuahidi kuchangia shilingi milioni
mbili.
Kwa
upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema tayari
CCM imeshajipanga vyema kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chambani.
‘’CCM
tunasema tuko tayari kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa ubunge wa imbo la Chambani
na hatuendi kushiriki tunaenda kushinda,’ alisema.
Hata
hivyo, alisema CCM itaendelea kushinda katika kila chaguzi zinazoandaliwa
nchini, kutokana na ubora na uimara wa sera zake kwa wananchi.
Nae
Katibu wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba wakati akiwasilisha taarifa ya mkoa ya
kichama katika skuli ya sekondari ya Fidel Castro, alisema CCM imejipanga vyema
katika kila jimbo ili kuhakikisha inaongeza idadi ya wanachama.
3 Comments
nakusikitia dr sheni kwa ulivyokuwa huna mtazamo wa kimaendeleo , zanzibar ilikotoka ilikuwa kuzuri , hapa tulipo sijui wapi gurudumu la maendeleo limejaa pancha za kila aina utatuambia nini? humwogopi aliye kuumba ambaye atakusimamisha siku ya siku ujibu dhuluma ulizosimamia juu ya wazanzibari? Kumbuka kusali sali na kufunga saumu za njaa hazimshughulishi mola , wala kufuturisha watu kwa fedha za haramu na dhuluma hazitokufikisheni popote , alie mbora ni yule mwenye kumwogopa mola tu na sio Kikwete au yoyote , serikali yako imejaa dhuluma na rushwa za kila aina , hakuna haki kama hukuinunua , unajisifu nini ? unacho cha kujisifu? nchi isiyozidi wilaya ya ilala mpaka leo imekushinda kuipatia umeme na maji , watu webebe ndoo na madumu kutafuta maji jee hayo ndio mafanikio yako? hospitali mbovu huduma hoi , mashuleni sikwambii hali , kama huoni basi ndio wale 'wana macho lakini hawaoni' Tena ikiwezekana tunawaomba wewe na kundi lako msijisogeze kwenye nyumba zetu za ibada , jengeni zenu mkasalishane na kufanya ibada zenu.
ReplyDeleteHawa viongozi wetu wanafanya kibri, hii ni chuki walinayo juu ya UAMSHO wasizunguke mbuyu waseme wazi kwani hilo liko wazi kwani hata bendera zenye kalima kubwa kuliko chochote wanaudhika wakiona zinapepea.Basi wanakumbushwa kwamba wamuogope yule ambaye ni ASSAMIU WALBASWIYR.
ReplyDeleteDr shen umecherewa umewacha mpaka wameota nabu, ndio mkachukua hatua pale walipo kuwa wanatembea na mapanga namitaimbo ulikuwa wapi hukutoa kauli na nchi ilkuwa ina elekea kubaya, sasa himiza vyombo vyenu vya ulinzi vikamilishe ushahidi kama kweli hamvumilii vurugu za dini siasa
ReplyDelete