Katibu wa Jumuiya ya Uvuvi na Mazingira Endelevu Zanzibar Hussen Makame akiwaonesha wanafunzi eneo la kupanda miti katika jitihada za kuzuia mmong’onyoko huko katika skuli ya msingi Mtoni kidatu juu.
Katibu wa Jumuiya ya Uvuvi na Mazingira Endelevu Zanzibar Hussen Makame na mwanafunzi Hafsa Juma wakipanda mti katika eneo la Skuli ya Mtoni kidatu juu
Mpiga picha wa Maelezo Zanzibar Makame Mshenga, akijumuika na wanajumuiya ya Uvuvi na Mazingira Endelevu Zanzibar katika zoezi la kupanda miti huko Skuli ya Msingi ya Mtoni kidatu juu.(Picha na Makame Mshenga Maelezo Zanzibar).
Na Miza Othman –Melezo Zanzibar 24/8/2013
Jumuiya ya Uvuvi na Mazingira Endelevu Zanzibar kwa kushirikiana na wanafunzi wa skuli ya Mtoni kitatu leo imeamua kufanya zoezi la upandaji wa miti kwa ajili ya kuzuia mmong’onyoko wa ardhi ambao unaoweza kuleta athari skulini hapo.
Hayo yaemeelezwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo baada yakufanya zoezi hilo huko skuli ya Mtoni kidatu nje kdogo ya mji wa Zanzibar.
Amesema lengo la kupanda miti hiyo ni kuyaendeleza mazingira pamoja na kuyadumisha ili kuwa endelevu katika skuli hiyo.
Nae Msaidizi wa Mwalimu Mkuu Hamdani Othman Skuli ya Mtoni amesema ikohaja ya kupandwa miti hiyo kwani skuli yao ipo juu ya mlima jambo ambalo linaweza kupelekea athari kwa wanafuzi wao.
“Skuli inaweza kuathirika na mazingira kwani iko juu ya malima kupanda miti itaondoa mmong’onyoko wa ardhi”,alisema Msaidizi Mwalimu Mkuu Hamdani Othman.
Katibu wa Jumuiya ya Uvuvi na Mazingira Endelevu Zanzibar Hussein Makame Mohamed amesema zoezi hili la upandaji miti ni muhimu katika maisha ya mwanaadamu kwani itapelekea kuenzi na kutunza mazingira ya watu wa Zanzibar.
“Lengo la kupanda miti ni baada ya kuona Zanzibar iko katika uharibifu wa mazingira ikiwa nchi kavu na baharini”,alisema Katibu Hussein Makame.
Ameongezea kusema pia Jumuiya ya Uvuvi na Mazingira Endelevu Zanzibar inalengo la kuwanyanyuwa vijana ambao waliokosa ajira na kuwawezesha kujiajiri katika Jumuiya hiyo.
Wanu Mlekwa Iddi ambaye ni mwana jumuiya hiyo amesema ameamuwa kujitolea na kujiumga katika Jumuiya hiyo katika kuyaenzi mazingira kwa ajili ya kulinda afya zao na mazingira yaliyo kwa jumla.
Hata hivyo amesema ni bora kupanda miti kwani itasaidia kuzuia udongo wakati wa mvua nyingi hasa katika skuli hiyo.
Jumuiya hio imeanzishwa 20 /1 /2012 tangu kuanzishwa inawanachama 22 hadi hisasa.
0 Comments