Kijiji cha Mzuri kinakumbwa na uhaba mkubwa wa upatikanaji wa maji. Kisima kikuu cha maji Makunduchi kimeishiwa nguvu. Pump iliyopo haina uwezo tena wa kusambaza maji Makunduchi nzima; tangi liliopo linavuja na hadi leo hakuna juhudi iliyofanjwa ya kuliziba.
Kutokana na shida hii wananchi sasa hawasubiri tena viongozi. Hivi sasa kuna juhudi za wananchi za kutafuta maji ya uhakika kijijini Mzuri kama gari hili liitwalo Chimba linavyoonekana likiwa kazini eneo la Kibondeni, Mzuri Kaja. Makunduchi.

Kinamama nao walikuwepo wakati wa uchimbaji wa kisima. Hapa wanaonekana wakisubiri kwa hamu habari ya upatikanaji ya maji kwani wao husumbuka zaidi na matatizo ya maji yanapoikumba jamii.
1 Comments
Ndugu mwandishi una uhakika kuwa hizo ni juhudi za wananchi???. Nijuavyo mimi Chimba Company ni contractor wa uchimbaji visima chin ya mradi wa uchimbaji visima Unguja na Pemba unaofadhiliwa na Ras El Khayma. Hepu turipotie kwa umakini.
ReplyDelete