6/recent/ticker-posts

Mwenyekiti wa ZFA Wilaya ya Mjini Chura Aipongeza timu ya Mkoa wa Mjinin Magharibi.

  Kombe la Ubingwa wa Michuano ya Coca Cola kwa Vijana chini ya Umri wa miaka 15, michuano hiyo imefanyika Mjini Dar es-Salaam na Timu ya Mkoa wa Mjini Magharibi kulichukuwa Kombe hilo kwa Mwaka 2013.kwa kuifunga timu ya Mkoa wa Temeke.
 
  Mwenyekiti wa ZFA Wilaya ya Mjini Hassan Chura akitowa salamu za pongezi kwa Wachezaji wa timu ya Mkoa wa Mjini Magharibi kwa kuchukua Ubingwa wa Kombe la COCA COLA zilizofanyika Mjini Dar-es-Salaam mwezi uliopita na kuibuka mshindi wa machuono hiyo, Tafrija hiyo iliandaliwa na Mwanyekiti huo Hassan Chura kwa wachezaji hao katika ukumbi wa Tawi la CCM Kilimani.
 Rais wa ZFA Taifa Zanzibar Rafia Idarous akitowa shukrani kwa ushindi wao wa Ubingwa wa Michuano ya Kombe la Coca Cola chini ya umzi wa miaka 17, zilizofanyika katika uwanja wa Karume Dar-es-Salaam. Tafrija hiyo imeandaliwa na Mwenyekiti wa ZFA Wilaya ya Mjini Hassan Chura, ili kuwapongeza Wachezaji hao kwa ushindi wao.

 Wachezaji wa timu ya Mkoa wa Mjini Magharibi wakiwa katika tafrija yao walioandaliwa na Mwenyekiti wa ZFA Wilaya ya Mjini Hassan Chura kwa ajili ya kuwapongeza kwa ushindi wao wa kulinyakuwa Kombe la Copa Coca Cola kwa mwaka 2013/2014


Post a Comment

0 Comments