Ujumbe wa wadi za Makunduchi uliofanya ziara ya kikazi kwenye manispaliti ya Kiruna nchini Sweden wakutana na wajumbe wa kamati za Maendeleo za Makunduchi kuzungumzia matokeo ya ziara hiyo. Wajumbe waliokaa kwenye meza kuu kutoka kushoto, karibu na televisheni ni afisa tawala ndugu Abdalla Ali Kombo, mwenye koti jeusi ni ndugu Moh'd Simba, Mw. Mwita Masemo na Mw. Haji Kiongo. Kwenye mkutano huo wa pamoja, wananchi wa Makunduchi wameelezea kuridhishwa kwao na jinsi walivyowakilishwa nchini Sweden. Mambo makuu yaliyokubaliwa kwenye ziara hiyo ni suala la elimu na visima vya maji. Ifikapo mwezi wa Januari mafunzo ya mwaka mmoja ya ujasiriamali kwa wanawake 12 yataanza rasmi. Aidha kituo cha mafunzo cha ICT cha Makunduchi kitawekwa vifaa vipya vikiwemo kompyuta 15, projectors pamoja na vifaa vya kuwezesha wanafunzi wakiwa Makuduchi kusoma kutoka kwa walimu waliokuwa Sweden (video conference facilities).
Wajumbe wa kamati za Maendeleo za Makunduchi wakifuatilia kwa makini ripoti ya ziara ya kikazi ya Manispaliti ya Kiruna, Sweden. Ripoti hiyo iliwakilishwa na mratibu wa ziara hiyo ndugu Mohamed Muombwa katika ukumbi wa mkuu wa wilaya ya Kusini Unguja. Katika mkutano huo zaidi ya maswala 20 yaliulizwa na kutolewa ufafanuzi wa kina
Wanafunzi waliosimama watakaopatiwa mafunzo ya ujasiriamali chini ya mradi wa elimu utakaoendeshwa chini ya mashirikiano kati ya wadi za Makunduchi na Manispaliti ya Kiruna watakiwa kuanza kujinoa kwa lugha ya kiingereza ili walimu watakapofika mwezi wa Januari 2014 kazi ya ufundishaji isiwe nzito. Wito huo ulitolewa na afisa tawala wa Wilaya ya Kusini, ndugu Abdalla Ali Kombo, ambaye pia amejitolea kulipia gharama za ufundishaji wa kiingereza cha kujiandaa na mafunzo ya mwaka mmoja.
0 Comments