Na Joseph Ngilisho,Arusha
KAYA 300 za watu wanaoishi na Ukimwi
zilizopo Halmashauri tatu mkoani Arusha, zinatarajia kufanyiwa utafiti juu ya
ukatili kwa watoto na kinamama waliopo ndani ya familia, ili kuangalia uwezekano
wa kupunguza ukatili huo.
Hayo yalisemwa jana jijini hapa na
Mratibu wa Ukimwi kutoka hospitali ya Selian, John Laizer, wakati akizungumza
na wadau mbalimbali waliojumuika kutoa mawazo yao juu ya vitendo vya ukatili,
vinavyofanywa na baadhi ya wanajamii.
Alisema
wanawake na watoto wanaoishi ndani ya familia, baadhi yao wanapata mateso
makubwa ya kupigwa,kudhalilishwa na kuvunjwa mikono, kutokana na baadhi ya
kinababa kuwa na tabia ya kuwapiga.
Alisema vipigo hivyo vinawaathiri kisaikolojia
watoto, hali inayosababisha kuwachukia baadhi ya wazazi wao, huku wengine
kukimbilia mitaani, kutokana na kuchukizwa na tabia za unyanyasaji.
Alisema
utafiti huo unatarajia kufanyika muda wowote kuanzia sasa na utajulikana kwa
jina la nyumba aminifu, utakaojumuisha halmashauri tatu za Arusha mjini, Arusha
vijijini na Monduli na utalenga kaya zilizoathirika
na Virusi vya Ukimwi.
Alisema utafiti huo utafanyika kwa
kushirikiana na Shirika la Savanna, Selian na kutumia viongozi wa mila na dini,
ili waweze kutoa ushirikiano na kupata majibu sahihi.
0 Comments