Na Kija Elias, Moshi.
MAMLAKA ya Udhibiti wa Chakula na Dawa
(TFDA), imelifunga kwa soko kuu la Moshi , baada ya kubainika kutokidhi viwango
vinavyotakiwa na hivyo kusababisha afya za watumiaji wa soko hilo kuwa hatarini kwa magonjwa ya mripuko.
Mamlaka hiyo iliagiza kufungwa kwa soko hilo kutokana na uchafu
uliokithiri na kwamba maeneo ambayo yanatolewa huduma ya kuuzia nyama ni
machafu mno.
"Mamlaka tumeamua kulifunga soko
hili kwa sababu ya afya za watu, soko ni chafu, halina miundombinu ya maji taka, na mabucha ya nyama ni machafu sana hayakidhi
viwango vya kutolea huduma,” alisema.
Kwa upande wao wafanyabiashara wa soko hilo, wamekiri kuwepo
uchafu ndani ya soko hilo, huku wakiitupia lawama ofisi ya Mkurugenzi wa
halmashauri kwa kushindwa kuwapa taarifa na hivyo kuwashtukiza huku wakiwa
tayari wamesha kopa mikopo mabenki,” walisema.
Wafanyabiashara hao ambao hawakutaka
majina yao yatajwe,wamedai agizo hilo
limekuwa la kushutukizwa na kwamba litasababisha hasara kubwa.
Aidha walisema kufungwa kwa soko hilo imekuwa
adhaabu kwao kwani wanatengemea biashara hiyo kuendeshea familia, ikiwemo
kuwasomesha watoto.
Akizungumzia suala hilo, Kaimu Mkurungenzi
wa Manispaa ya Moshi, Dk. Christopher
Mtamakaya, amekiri kuwepo taarifa
za kufungwa soko hilo .
Alisema manispaa hiyo imetenga
fedha zaidi ya shilingi milioni
200 kwa ajili ya ukarabati wa soko hilo, ambapo kwa sasa wako katika hatua za
kumpata mkandarasi.
Alisema wafanyabiashara hao watahamishwa
katika soko la Kiusa ambalo limefanyiwa ukarabati na lina nafasi kubwa ili kupisha ukarabati.
Meya wa manispaa ya Moshi, Jafari
Michael, ametofautiana na Mkurugenzi huyo kwa madai fedha zilizotengwa kwa ajili
ya kukarabati soko hilo
ni shilingi milioni 75 ambapo hadi
ukarabati kukamilika zinahitajika shilingi milioni 280.
Alisema ni vyema manispaa ikatafuta
utaratibu mzuri wa kuwaondoa wafanyabiashara kuliko kutumia utaratibu ambao
wameutumia wa kuwafungia kabisa wasifanye biashara.
Kwa upande wake diwani kata
ya Kaloleni, Michael Mwita, alisema
barazala madiwani, halijawahi kujadili
suala hilo
0 Comments