Na
Mwandishi wetu
CHAMA
cha Wanahabari Wanawake Tanzania
(TAMWA) leo kitazindua ripoti ya utafiti wa unyanyasaji wa kijinsia uliofanyika
Disemba 2013 katika wilaya 20 za Tanzania
Bara na Zanzibar .Uzinduzi
huo utafanyika ofisi za TAMWA Sinza Mori Dar es Salaaam.
Uzinduzi
huo ni kutokana na utafiti uliofanyika baada ya mafunzo kutolewa kwa waandishi
wa habari juu ya habari za uchunguzi dhidi ya ukatili wa
kijinsia kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya
watu (UNFPA).
Ripotii
hiyo inaonyesha hali halisi ya unyanyasaji wa kijinsia katika jamii pamoja na
mambo yanayokwamisha juhudi za vyombo vinavyotetea haki za wanawake na watoto
nchini.
Utafiti
huo ulifanywa kwa kushirikiana na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali
vya Zanzibar Leo, Nipashe, The Guardian, The Citizen, Mwananchi, Daily
News, Majira na Kituo cha Televisheni cha ITV.
Taarifa
ya TAMWA ilisema katika utafiti huo waandishi wa habari waliweza kuwahoji
wanajamii mbalimbali kuanzia ngazi za familia na kupata ukweli wa hali halisi ya
unyanyasaji wa kijinsia ikiwemo, ukeketaji, ubakaji, mauaji ya vikongwe, mimba
katika umri mdogo na watoto wa kike kulazimishwa kuolewa.
Wilaya
ziliyofanyiwa utafiti ni Kahama, Tarime, Sengerema, Newala, Mbulu, Singida
Vijijini, Bariadi, Busega, Nkasi, Dodoma, Babati, Chunya na Bunda.
Kwa
upande wa Zanzibar utafiti ulifanywa katika wilaya sita za mikoa ya mjini magharibi,
kusini Pemba, kaskazini Pemba, Unguja kusini na kaskazini Unguja.
0 Comments