Na Madina Issa
MKUU wa
Mkoa wa Mjini Magharibi,Abdalla Mwinyi Khamis, amesema kuanzishwa kituo cha
utoaji taaluma cha Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), kutawawezesha wafanyakazi
kufanya kazi kwa uhakika.
Aliyasema
hayo alipofungua kituo hicho kilichopo Mtoni.
Alisema
ni vyema kwa mamlaka hiyo kuendeleza jitihada zao ili kituo hicho kiweze kutoa
fursa nyengine za elimu.
Aidha
alisema azma ya ZAWA kuanzisha kituo hicho ni kuinua kiwango cha elimu cha wafanyakazi wake ili kufanya kazi kwa ufanisi.
Alisema
azma ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar za awamu zote ilikuwa ni kuinua hali za
wananchi kwa kuwawezesha wakulima na wakwezi kushiriki katika uendeshaji wa
serikali yao .
Akizungumzia
suala la maji safi na salama, alisema serikali ilipitisha sera ya taifa ya maji
ya mwaka 2004 ikiwa na dhamira ya kuweka misingi madhubuti ya kusaidia kuandaa
mikakati ya kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma hiyo.
Aidha
alisema dhamira hiyo pia ilienda sambamba na kuanzishwa kwa sheria namba tano
ya mwaka 2006 sheria ambayo imepelekea kuanzishwa kwa chombo makhsusi cha
kusimamia rasilimali za maji na usambazaji wa huduma hiyo kwa wananchi wote.
Hata
hiyo, alisema hali ya upatikanaji wa maji safi
kwa wananchi inaridhisha ikilinganishwa na hapo awali ambapo zaidi ya asilimia
75 ya wananchi wanaoishi mijini na asilimia 65 ya wanachi wai vijijini
wananufaika moja kwa moja na huduma hiyo.
Hivyo
aliwataka viongozi wa mamlaka hiyo kuendelea kuelimisha wananchi kuhusu hatua
mbalimbali zinachukuliwa na serikali kuwapatia wananchi huduma ya maji safi na salama.
Hata
hivyo, aliliomba ZAWA kukitunza kituo hicho na kukiendeleza zaidi ili
kuhakikisha kinakuwa endelevu kwa dhamira ya kuimarisha uwezo na ufanisi wa
watendaji wa mamlaka hiyo.
Nae
Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Dk. Mustafa Ali Garu, akitoa taarifa ya kitaalamu
alisema kuanzishwa kwa kituo hicho ni miongoni mwa jitihada za serikali na
mamlaka kuwapatia elimu wafanyakazi kulingana na fani zao.
Kituo hicho cha taaluma cha Mtoni kimegharimu zaidi ya
shilingi milioni 5 ukiwa ni ufadhili wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB), Shirika la Makaazi Duniani (UN- Habitat) na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
ambapo jumla ya wafanyakazi 30 wameanza ku
0 Comments