Asha
Salim na Maryam Salim, Pemba.
WANANCHI
wa Mkoa wa Kusini Pemba, wameeleza kilio chao cha kukosa huduma ya televisheni
zote kupitia king’amuzi vya ZBC, jambo ambalo linawatia hofu na kusababisha
wengi wao kuogopa kununua ving’amuzi.
Wananchi
hao walieleza kilio hicho kwa nyakati tofauti wakati wakizungumza na mwandishi
wa habari hizi..
Walisema
kwa sasa wamepoteza tamaa kupata matangazo ya aina yoyote kupitia runinga hali
inayosababisha kushindwa kupata taarifa zinazotokea duniani.
Walisema
inadhihirisha serikali haikujipanga kuingia katika mfumo wa dijitali huku
wakisema wameingia hasara kununua ving’amuzi visivyo na tija.
Mmoja
kati ya wananchi hao, Ramadhan Salim Khamis, alimwambia mwandishi wa habari hii
kwamba alilipa shilingi 75,000 kununua king’amuzi na ada ya shilingi 8,000 kila
mwezi.
Kwa
upande wake, Seif Nassor Seif, aliiomba serikali kupitia taasisi husika kuandaa
utaratibu maalum unaotambulika kuanzia ununuzi wa ving’amuzi hadi kulipia
gharama kwa wateja ambao hawapati huduma yoyote.
Ofisa
Mdhamini Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii
na Michezo Pemba, Ali Nassor Mohammed, alikiri kuwepo kwa tatizo na
kusema limesababishwa na upepo uliovuma hivi karibuni.
Hata
hivyo, alisema mafundi wanaendelea na matengenezo ili wananchi wapate tena
huduma.
0 Comments