Na Mwandishi Wetu.
Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko imekiri kuwepo kwa
malalamiko kutoka kwa Wakulima wa zao la Karafuu, Wananchi na wauzaji wa
karafuu hasa kisiwanin Pemba kwamba wanapouza
na kupimiwa karafuu zao kituo cha ZSTC zinapofikia bakaaya nusu au robo huwa
hawalipwi na badala yake hulipwa kilo nzima.
Naibu Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe. Thuwaiba
Kisasi,aliyasema hayo katika baraza la Wawakilishi wakati ajibu suala la
mwakilishi wa Jaku Hashim Ayoub,(Muyuni) aliuliza kwa nini Serekali haitowe
kauli juu ya malalamiko hayo ya Wakulima wa Zao la Karafuu na Wauzaji wa
karafuu kupata hakin yaohata kama ni kiwango kidogo.
Waziri Kisasi alisema baada ya Wizara hiyo
kufuatiliamalalamiko hayo imegunduwa kuwa malalamiko hayo hayana ukweli kwa
sababu mezani zinazotumiwa na Shirika la ZSTC kwa kupimia karafuu wakati
wanapozinunua zina vipimo vyote kuaznzia kilo moja hadi robo kilo na zinatumika
ipasavyo.
Katika kuhakikisha mauzo hayo yana kumbukumbu za ununuzi wa karafuu
za kila siku na za kila mkulima anaekwenda kuuza karafuu katika kiwango
chochote kile huwa zinaingizwa katika daftari la manunuzi katika kituo hicho.
Aliliambia baraza hilo .
Hata hivyo, alisema kwa bakaa ya karafuu ambazo ni kidogo
kiasi kwamba hadhikidhi kiwango cha robo kilo Shirika la SZTC humrejeshea
mkulia mwenyewe karafuu hizo na sambamba na hayo alisema kuwa shirika la SZTC
.Litaendelea na kuchukuwa jitihada za kuwaelimisha zaidi wakulima wa karafuu
ili waelewe vipimo sahihi vinavyotumika katika kupima mazao au karafuuzao.
0 Comments