Na Mwandishi Wetu.
Jumla ya shilingi milioni 400,000,000 zimetengwa kwa ajili
ya programu maalum ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabia Nchi kwa
mwaka wa Fedha 2014/2015.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza
wa Rais Mhe. Fatma Ferej Abdulhabib, amesema kuwepo kwa mabadiliko ya tabianchi
kuwa kubwa kumesababisha kutengwa kwa fedha hizo ili kukabiliana na hali hiyo.
Aidha alisema katika kipindi cha miaka miwili iliopita jumla
ya shilingi1,316,752,700.0, zimeshatumika
kwa shughuli mbalimbali za kukabiliana na mabadiliko tabianchi kupitia
taasisi sita zinazohusika katika kutekeleza mradi huo.
Alisema fedha hizo zitapatikana kupitia programu ya
kuendeleza Utalii Zanzibar na zitalenga zaidi katika kuendeleza ustawi na
matumbawe ambayo yamekuwa yakiathiriwa na kupanda kwa joto la bahari na hatimae
kufa hali ambayo imekuwa ikileta usumbufu kwa wavuvi pamoja na kupunguza haiba
kwa watalii.
Waziri Fatma alieleza hayo katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi
wakati akijibu suala la Mwakilishi wa jimbo la Wawi, Mhe. Saleh Nossor Juma,
alitaka kujua ni kiasi gani Serekali
imepanua Bajeti ya Idara ya Mazingira katika suala zima la la kupambana na
mabadiliko ya tabianchi Zanzibar .
’’Serekali inaelewa kuwa kiasi hicho cha fedha ni kidogo mno
kukidhi mahitaji lakini hata hivyo imeamua kuaza kwa uwezo wake mdogo na
kuendelea kufanya hivyo kadri hali itakavyoruhusu, ili kuhakikisha
Zanzibar inakuwa na uhakika wa upatikanaji
wa fedha za mabadiliko ya tabianchi’’ alisema Waziri huyo.
Alisema katika kupambana na suala hilo pia Serekali imeanda mradi na
kuhamasisha rasilimali za kuweza kutekeleza mradi huo.
Alifahamisha kwa kutambua suali la mabadiliko tabianchi ni
kubwa linalohitaji fedha nyingi kulishughulikia Serekali ya Mapinduzi Zanzibar
imeona ipo haja ya kuanzisha mradi huo ambao mwaka 2012 ilitiliana saini na
Shirika la UNDP kupitia programu ya UNDP,kwa ajili ya kuuendesha mradi huo.
Hata hivyo alisema lengo kuu la mradi huo ni kujenga uwezo
wa kuhimili na kusimamia mabadiliko tabianchini tatizo kubwa linaloikabili
dunia hivi sasa ambapo nchi za visiwa kama Zanzibar ni maeneo ambayo yako hatarini zaidi
kuathiriwa na athari hizo.
Pia alisema sekta mbalimbali za kiuchumi, kijamii na
kimazingira zimekuwa zikiathirika kwa kiasi kikubwa, kwani mabadiliko ya
tabianchi yamekuwa ni tishio kwa maendeleo endelevu ya dunia na kikwazi kikubwa
cha kufikia malengo ya melenia yaliyowekwa.
Waziri alibainisha chanzi kikuu cha kutokea kwa athari hizo
ni kuongezeka kwa gesi ya ukaa kwenye usawa wa dunia.
Hata hivyo alisema Serekali imekuwa ikiendeleza jitihada
mbalimbali za kuhakikisha kuwa mitaala ya skuli za msingi hadi vyuo vikuu
inahusisha masuala ya mazingira ambapo kwa kuanzia Serekali imeingiza somo la
mazingira katika ngazi ya msingi hadi Sekondari.
0 Comments