Na Bakar Mussa, Pemba
Walimu wa Ushauri Nasaha Kisiwani Pemba,
wameshauriwa kuwa karibu sana na Wazazi wa Wanafunzi hasa wale wenye tabia
zisizo za kawaida ili kuweza kupata mafanikio ya haraka ya kuwabadilisha tabia
zao.
Akizungumza na Walimu wa Ushauri Nasaha kwa
Skuli 53 za Kisiwani humo huko katika Skuli ya Sekondari Madungu,Afisa wa kitengo
cha Stadi za Maisha kutoka Wizara ya Elimu Pemba, Khamis Haji Hamad ,
alisema kuwa Bakora sio suluhisho linaloweza kumbadilisha tabia mtoto wa aina
hiyo na badala yake Ushauri Nasaha unaweza kumuweka pazuri zaidi.
Afisa huyo alifahamisha kuwa Walimu hao
wanamchango mkubwa wa Malezi iwapo watakuwa bega kwa bega na Wazazi jambo ambalo linaweza kumuepusha Mtoto wa
aina hiyo kuwa mzigo kwa wenzake na Wazazi wake .
Halima Ali Ahmada, Mratibu wa Ushauri Nasaha
WEMA Pemba, aliwataka Walimu hao kutowa Mafunzo hayo kwa Wanafunzi wao kwani
lengo la kuwepo kwao ni kuwapa Ushauri mbali mbali Wazazi na Walimu ili kuepuka
na kujiingiza katika matendo maovu na hatarishi.
Alisema kuwa ni vyema Walimu hao kuwa
karibu sana na Wazazi wa Watoto bila ya woga ili kuwepo mashirikiano ya pamoja
ya malezi yenye maadili mema ambayo hayatakuwa na Vishawishi.
Kassim Hamad Khamis, Mwalimu Mkuu wa Skuli
ya Mkia wa Ng’ombe Pemba, alieleza kuwa mafunzo yatawasaidia sana kwa vile
wamekuwa wakikaa pamoja na Watoto wenye tabia na Mazingira tafauti ambazo
zinaweza kurekebishika kwa kuwapa Ushauri Nasaha.
“ Mbinu tunazopatiwa za Ushauri Nasaha
zinaweza kutusaidia vya kutosha kwa kujenga Taifa lenye Vijana wenye Maadili
mema”,alisema.
Alifahamisha kuwa Ushauri Nasaha ni muhimu
zaidi kumfukuza mtoto kuliko Bakora kwa Vile zinamfanya mtoto kuwa Mkaidi
zaidi.
Nae, Mwalimu wa Ushauri Nasaha wa Skuli ya
Msingi Vitongoji ,Mkunga Hamad Sadala, alisema kuwa Wanafunzi sasa hivi
wamekuwa wakijiingiza katika mambo mbali mbali ya Anasa kama vile Mapenzi ya ya
Umri mdogo, madawa ya kulenya nk, hivyo mafunzo hayo wanayopatiwa
mara kwa mara yatawasaidia kuwatowa Wanafunzi katika Dimbwi hilo hatarishi hasa
wale wanaoingia katika rika la Utuuzima(Balekhe).
“Mafunzo haya ya mara kwa mara
tunayopatiwa yanatusaidia sana ili kukabiliana na Watoto wenye wenye Changamoto
na Vishawishi mbali mbali vya Kimaisha,” alisema Mkunga.
Hivyo alisema kuwa Suala la Mapenzi kwa
Wanafunzi ni tatizo kubwa na kama sio
mafunzo hayo ya Ushauri Nasaha wanayopatiwa Taifa lingekuwa hali mbaya zaidi.
0 Comments