Na
Fatina Mathias, Dodoma
WATU
wawili wamefariki dunia wilayani Mpwapwa mkoani hapa kwa kupigwa katika matukio
mawili tofauti.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, David Misime, alisema
tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa tano na nusu usiku katika kijiji
Mzogole.
Alisema
mkazi wa Mzogole Richard Kodi (55) aliuawa kwa kupigwa na wananchi baada ya
kumuua mkewe Mwajuma Chomola (48) kutokana na wivu wa mapenzi.
Kamanda
huyo alisema marehemu Mwajuma aliuawa kwa kupigwa rungu tumboni upande wa
kushoto na mume wake huyo.
“Baada
ya Mwajuma kuuawa Richard naye aliuawa siku iliyofuata majira ya saa tatu
asubuhi kwa kushambuliwa na wananchi waliojichukulia sheria mkononi na
alifariki dunia,”alisema.
Alisema
marehemu Richard alifariki akiwa anaendelea na matibabu katika hospitali ya wilaya
ya Mpwapwa.
Alisema
uchunguzi wa awali unaonesha chanzo cha mauaji hayo
ni wivu wa mapenzi.
Alisema
Mwajuma aliuawa baada ya kuchelewa kurudi kutoka kwenye sherehe iliyokuwa hapo
kijijini akidhani kuwa ameenda
kwenye masuala mengine.
Aidha
alisema jeshi la polisi bado linawatafuta wananchi waliojichukulia sheria
mkononi ili wafikishwe mahakamani.
0 Comments