Na
Hanifa Salim, Pemba
WANANCHI
wa shehia ya Matale wilaya ya Chake Chake mkoa wa kusini Pemba, hawana kituo
cha afya kwa miaka mingi sasa.
Walisema
wamekuwa wakipata usumbufu wa kuitafuta huduma hiyo.
Mmmoja
kati ya wananchi hao, Siasa Khamis Ali, alisema katika kijiji chao kituo cha
afya ndio changamoto kubwa ambayo inawakabili na kwamba serikali inapaswa
kulipatia ufumbuzi.
Nae
Mkubwa Juma Abdalla, alisema tokea Mapinduzi ya mwaka 1964, hawajawahi
kujengewa kituo cha afya.
Aliiomba
serikali na viongozi wa ngazi za juu kuwaangalia kwa jicho la huruma ili
kuhakikisha kituo cha afya kinajengwa.
Mkuu
wa Wilaya ya Chake Chake, Hanuna Ibrahim Masuod, alisema tatizo hilo litapatiwa
ufumbuzi kwa ushirikiano na wananchi.
Msaidizi
Sheha wa shehia ya Matale, Mwalimu Haji Mchande, aliiomba serikali na viongozi
wa ngazi ya juu kusikia kilio chao cha muda mrefu.
2 Comments
Tokea mwaka 1964 hamjajengewa kituo cha afya poleni sana. Lakini fikirieni Plan B najua mnaweza jengeni wenyewe hicho kituo na serikali muidai daktari na madawa.
ReplyDeleteTokea mwaka 1964 hamjajengewa kituo cha afya poleni sana. Lakini fikirieni Plan B najua mnaweza jengeni wenyewe hicho kituo na serikali muidai daktari na madawa.
ReplyDelete