Mgombea Urais wac Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Mhe Mohammed Msoud Rashid akiwasilui katika viwanja wa Afisi ya Tume Bwawani Zanzibar kwa ajili ya kuchukua Fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibar akiongozana na Wanachama wake.
Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Salum Kassim Ali akitowa maelezo wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi fomu ya Kugombea Urais kabla ya kumkaribisha mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar kukabidhi fomu hiyo.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Jecha Salum Jecha akisoma fomu ya kujazwa kwa wagombea wa Urais wa Zanzibar kabla ya kumkabidhi Mgombea kuzingatia masharti ya ujazaji wa fomu hiyo.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Jecha Salum Jecha akionesha mkoba wa Fomu za Urais kabla ya kumkabidhi Mgombea wa Chama cha (CHAUMMA) Mhe Mohammed Masoud Rashid.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Jecha Salum Jecha akimkabidhi fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar Mgombea wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Mhe Mohammed Masoud Rashid,hafla hiyo imefanyika katika Afisi za Tume ya Uchaguzi Ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe Mohammed Masoud Rashid akionesha mkoba wake uliokuwa na fomu ya kuwania urais wa Zanzibar baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Jecha Salum Jecha katika Afisi za Tume Bwawani Zanzibar
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha CHAUMMA akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali baada ya kuchukua famu hiyo ya kuwania Urais wa Zanzibar.akiwa nje ya ukumbi wa Salama Bwawani.
Mgombea Urais kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Mhe Mohammed Masoud Rashid, akitoka Afisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar zilioko katika Hoteli ya Bwawani Ukumbi wa Salama baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Masoud Rashid akiwa na mkoba wake wa Fomu ya Kuwania Urais wa Zanzibar baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar.
1 Comments
Sasa jambo ninalonishangaza kuwa unajua fika kuwa hufiki popote sasa yanini kuengeza idadi!! si afadhali ukatizama chama gani kikubwa chenye nguvu ukakiunga mkono kuongeza NGUVU.
ReplyDelete