Matthew Rycroft, Mwakilishi wa Kudumu wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa na Rais wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, kwa mwezi Novemba, akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani, mara baada ya Baraza Kuu la Usalama kumaliza kikao chake kilichojadili hali ya Burundi, kikao ambacho pia kilipitisha azimio ambalo pamoja na mambo mengine linamuunga mkono Rais wa Uganda Yoweri Museven ambaye aliteuliwa na Viongozi wenzie wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa msimamizi na mwezeshaji wa majadiliano kati ya pande zinazopinga nchini Burundi.
Na Mwandishi Maalum, New York
Baraza
Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa
limelaani vikali hali ya kuendelea kwa matukio ya mauaji, utesaji na
vitendo vingine vya vinavyokiuka haki za
binadamu nchini Burundi.
Pamoja
na kukemea hali hiyo, Baraza Kuu la
Usalama limeeleza kusudio la kuchukua hatua zaidi kwa nchi hiyo
ya Burundi. Pamoja na
kumwomba Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa, katika kipindi cha siku kumi na
tano awasilishe mbele ya Baraza hilo taarifa kuhusu uwepo wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi katika siku za baadaye.
Jana
( Alhamisi) Baraza hilo lilikutana
katika kikao chake cha 7557 ajenda ilikuwa ni Burundi ambapo, Baraza kwa kauli moja lilipitisha Azimio namba 2248 (2015).
Kupitia Azimio hilo, Baraza limetoa wito
kwa pande zote nchini Burundi kujiepusha
na kukataa fujo ikiwa ni pamoja na kujiepusha
na vitendo vyovyote vinavyoweza kutishia
Amani na utulivu wa taifa hilo.
Vile Vile Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa
Mataifa ambalo kwa mwezi huu wa
Novemba Rais wake ni Uingereza
limekema vikali kauli za uchochezi
zinazotolewa na baadhi ya watu ndani na
nje ya Burundi, kauli ambazo kwa mujibu
wa Baraza hilo zinalenga katika kushawishi chuki baina ya makundi ya watu nchini humo.
Kufuatia
kauli hizo za uchochezi, Baraza
Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa,
limeitaka Serikali ya Burundi kuheshimu, kulinda na kuhakikisha haki za
binadamu na misingi ya uhuru, kuheshimu utawala wa sheria pamoja na uwajibikaji
wa uwazi dhidi ya fujo na itoe ushirikiano kwa Ofisi ya Kamisheni ya Haki za Binadamu.
Kupitia
Azimio hilo Baraza Kuu pia limeitaka serikali ya Burundi kuwawajibisha
wale wote watakaopatikana na hatia ya
ukiukwaji ya Sheria ya Kimataifa ya haki za binadamu na unyanyasajji wa haki za
binadamu.
Aidha kupitia
Azimio hilo, Baraza Kuu la
Usalama limetoa wito kwa Serikali ya
Burundi kutoa ushirikiano katika majadiliano yanayoongozwa na Jumuiya ya
Afrika Mashariki na ambayo yameridhiwa na Umoja wa Afrika na
limetaka kuitishwa haraka majadiliano
yatakayokuwa jumuishi yakiwashirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya
Burundi ili kutafuta muafaka
utakaokubaliwa na pande zote.
Baraza
Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa pia kupitia Azimio hilo limesema linamuunga
mkono kwa nguvu zote mwezeshaji wa majadiliano hayo ambaye ni Rais Yower Museveni wa Uganda
aliyeteuliwa na Viongozi wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki.
Katika kusaidia mchakato wa majadiliano hayo, Baraza Kuu la
Usalama la Umoja wa Mataifa
limemkaribisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
kupeleka timu ya wataalam ambao kwa kushirikiana na Serikali, Umoja wa Afrika na wadau wengine
watabuni mbinu
za kushughulikia matatizo ya
kisiasa na kiusalama.

0 Comments