Na Hawa Abdallah
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema imeipa kipaombele suala la haki za watu wenye ulemavu kwa kuanza kuchukua hatua za makusudi ili kufikia kuwa na jamii jumuishi hapa nchini pamoja na kuhakikisha kwamba watu wenye ulemavu wanamudu maisha yao,
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu Zanzibar Ussi Khamis Debe wakati akisoma hutuba kwa niaba ya Waziri wa nchi ofisi ya Makam wa kwanza wa rais katika uzinduzi wa Program na shughuli mbalimbali kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya watu wenye ulemevu Duniani ambapo kwa Mwaka huu kwa Zanzibar yatafanyika Kisiwani Pemba Disemba 3.
Alisema miongoni mwa mambo ambayo serikali yameyapa kipaumbele ni Kutungwa kwa Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali zinazosimamia haki za watu wenye ulemavu Nchini.
Kuundwa kwa Baraza la Taifa na Mabaraza ya Wilaya ya watu wenye ulemavu, Kuanzishwa kwa mfuko wa Maendeleo ya watu wenye ulemavu ambapo tayari umeanza kufanya kazi za kuwahudumia watu wenye ulemavu.
Alisema Kuendelea kusimamia upatikanaji wa miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu kwa kuanza kukagua majengo mbalimbali ya umma na binafsi pamoja na kujenga Skuli mbili mahususi kwaajili ya watu wenye ulemavu huko Jengele na Pujini.
Aidha alisema serikali imetenga fedha kupitia Wakala wa uwezeshaji wananchi Kiuchumi zinazotokana na makusanyo ya halmashauri kwa umaarufu 4-4-2.
Hata hivyo alisema katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya watu wenye ulemavu, Wizara hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imepanga kufanya shughuli kadhaa ikiwa ni shamra shamra za shughuli hizo.
Alisema miongoni mwa shughuli hizo ni, kufanya uhamasishaji kupitia vyombo vya habari, Michezo ya watu wenye ulemavu, Upimaji wa afya, maonyesho ya bidhaa za watu wenye ulemavu pamoja na Kilele cha Maadhimisho ambacho tunatarajia kufanyika kisiwani Pemba kwa mwaka huu.
Aidha, amewaomba wanajamii kushiriki kikamilifu na kuzitumia fursa hizo katika kuhakikisha wanaongeza uelewa kuhusu masuala ya ulemavu,
Hata hivyo aliitaka Jamii na watu wenye ulemavu kuwa mwaka 2025 katika kuelekea uchaguzi mkuu hivyo aliwataka kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo na kuhakiki taarifa zao katika daftari la kudumu la wapiga kura, kwani ni moja ya miongoni mwa haki za msingi,
Alisem kwa wale ambao hawaja jiandikisha wajitokeze kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ili kupata fursa katika uchaguzi mkuu kuwachagua viongozi ambao watakwenda kuleta mapinduzi makubwa katika kuijenga Zanzibar kwenye sekta ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni na kuhakikisha maendeleo yanaendelea kupatikana.
Aliwaomba watu wenye ulemavu kuwa na uthubutu katika kugombania nafasi mbalimbali za kiuongozi, kuanzia wadi hadi Taifa.
Hata hivyo alilishukuru Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu pamoja na wadau wote wakiwemo Taasisi ya Zanzibar Initiative Organization (ZIO) kwa kuandaa hafla hiyo adhimu, sambamba na Kuwashukuru Shirikisho la Jumuiya za Watu wenye Ulemavu Zanzibar (SHIJUWAZA) na jumuiya zake zote,na wadau kutoka Madrasa Early Childhood Programme na NAD pamoja na watendaji wote kutoka Ofisi yake.
Nae Afisa utawala kutoka taasisi ya Zanzibar Initiative Organization Twalaa Juma Khamis alisema Waandishi wa habari Wananchang mkubwa katika kuelimisha jamii kuhusu maswala ya watu wenye ulemavu.
Hata hivyo alisema katika kuelekea maadhimisho hayo taasisi hiyo itashiriki kikamilifu kuanzia proramu zote ambazo zimeandaliwa ili kuwahamasisha watu wenye ulemavu kupitia shughuli za mbalimbali wanazozifanya.
0 Comments