Meya wa Jiji la Zanzibar, Kamal Abdulsatar Haji leo asubuhi ameongoza zoezi la ukataji miti pembezoni mwa Barabara iliyozidi urefu katika maeneo ya Majumba ya Serikal ya Michenzani kwa lengo la kuweka haiba na mazingira mazuri Jiji la Zanzibar.
Katika zoezi hilo pia alishiriki Meya wa Manispaa ya Mjini, Muhamed Ibrahim Hassan, Madiwani wa Baraza la Jiji pamoja na Watendaji, sambamba na hilo Kamal amesema ofisi yake ina mipango madhubuti ya kuhakikisha kuwa Jiji linabaki safi na salama kwa vile Zanzibar ni kitovu kikuu cha Utaliii.




0 Comments