KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais Fedha Uchumi Mipango na Maendeleo Khamis Mussa akitia saini kwa niaba ya Serekali ya Mapinduzi Zanzibar na Balozi wa Japan Nchini Tanzania Hiroshi Nakagawa akisaini kwa niaba ya Sedrekali ya Japan, utiaji wa saini huo umefanyika hoteli ya serena inn shangani.
MANEJA Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar Hassan Ali Mbarouk mwenye suti na Maofisa wa Shirika hilo wakishughudia utiaji wa saini huo, uliofanyika Hoteli ya Serena Shangani.
KATIBU Mkuu wa Ofisi ya Rais Fedha Uchumi na Maendeleo, Khamis Mussa na Mwakilishi wa JICA Yukihide Katsuta wakitiliana saini kwa niaba ya Taasisi zao kwa ajili ya Usambazaji wa Umeme Unguja.
KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais Fedha Uchumi na Maendeleo Khamis Nussa na Mwakilishi wa JICA Yukihide Katsuta wakibadilishana mikataba baada ya utiaji wa saini ya ushambazaji wa umeme Unguja.
KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais Fedha Uchumi na Maendeleo Khamis Mussa akitowa shukrani baada ya utiaji wa saini wa msaada wa Mradi wa Usambazaji wa Umeme Unguja, sherehe hizi zimefanyika hoteli ya Serena Shangani.
BALOZI wa Japan Nchini Tanzania Hiroshi Nakagawa akizungumza baada ya utiaji wa saini Mradi huo
MWAKILISHI wa JICA Yukihidi Katsuta akizungumza baada ya kutia saini mradi huo, akitowa maelezo ya utekelezaji wake mradi huo wa usambazaji wa Umeme Zanzibar.
WATENDAJI wa Wizara ya Fedha, Uchumi na Maendeleo na wa Wizara ya Ardhi na Makazi wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Japan baada ya kumaliza kutia Saini Mradi wa Usambazaji Umeme Zanzibar.
No comments:
Post a Comment