Habari za Punde

ZEC KUZISHUGHULIKIA KASORO ZA UCHAGUZI

Yaahidi uchaguzi ujao kuwa wa kidemokrasia

UNDP yaridhishwa na matumizi ya misaada

Yunus Sose, STZ

MWENYEKITI wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Khatib Mwinchande, amesema anamatumaini makubwa kuwa Tume hiyo itafanya kazi zake kwa ufanisi katika uchaguzi mkuu ujao.

Alisema anajipa imani hiyo kutokana na kasoro nyingi zilizojitokeza katika uchaguzi uliopita mwaka 2010 kupatiwa ufumbuzi.

Alifahamisha kuwa pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika uchaguzi uliopita lakini kulijitokeza baadhi ya kasoro zilizosababishwa na mambo mbali mbali ambazo zinaweza kupatiwa ufumbuzi.

Alifahamisha kuwa lengo la kuzifanyia kazi kasoro zilizojitokeza ni kutaka kuhakikisha kuwa uchaguzi wa Zanzibar unakuwa wa huru, wa haki na wenye mazingira ya kidemokrasia.

Mwinchande alieleza hayo alipokuwa alipokuwa akitoa ufafanuzi wa hoja, maoni na ushauri kutoka kwa washiriki wa Kongamano la Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, lililofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar ocean View.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.