BODI ya Ushauri ya Hospitali Binafsi imevifungia vituo viwili vya afya vya binafsi baada ya kubainika kuwa na kasoro mbali mbali kufuatia ukaguzi uliofanyika hivi karubuni.
Vituo hivyo ni pamoja na Altabibu Dispensary iliyopo maeneo ya Magogoni na Huduma Dispenasary iliyopo maeneo ya Muembemakumbi.
Msaidizi Mrajis wa Bodi hiyo Dk. Shaaban Seif Mohammed alisema kasoro walizozibaini katika ukaguzi walioufanya ni pamoja ukosefu wa wafanyakazi wa kutosha na wenyesifa ya kutoa huduma katika hospitali ya Altabibu.
Alisema katika hospitali ya Huduma kasoro zilizokuwepo ni pamoja na uchafu katika chumba cha kupigia sindano na chakufungia vidonda na wafanyakazi wake hawana vyeti vya kufanyia fani ya afya pamoja na ukosefu mkubwa wa maji katika hospitali hiyo.
Alifahamisha kuwa bado wataendelea na zoezi la kufanya ukaguzi wa vituo binafsi vya afya kwa lengo la wamiliki wa Hospitali hizo kutoa huduma bora za afya kwa wananchi na kuepuka madhara yasitokee.
Alisema kuna baadhi ya vituo hivyo wanakaguliwa na wanapokutwa na mapungufu hufungiwa na baadae wamilikmi hufungua hospitali zao kinyemela jambo ambalo kisheria halikubaliki.
Amesema hivi sasa wanashirikiana na jeshi la polisi katika kazi zao iwapo mmliki atafungua kinyemela baada ya kufungiwa bodi kwa kushirikiana na jeshi hilo litamchukilia hatua mmiliki yeyote atakaefanya hivyo
No comments:
Post a Comment