Habari za Punde

SMZ KUENDELEA KUDHIBITI ZAO LA KARAFUU

WIZARA ya Biashara, Viwanda na Masoko, huwapandishia bei ya zao la karafuuu kadri soko linavyokuwa katika dunia na uwezo wa Serikali inaporuhusu.

Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Thuwaiba Edington Kissasi alilieleza Baraza la Wawakilishi alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mohammed Mbwana Hamad. (Chambani)

Naibu huyo alisema wizara yake imekuwa ikipandisha bei ya zao la karafuu kwa wakulima mara kwa mara kulingana na hali ya bei kwenye soko la dunia.

Alisema Januari Mosi mwaka huu wizara yake ilipandisha bei ya karafuu kutoka shilingi 4,000 na kuweka shilingi 5,000 kwa daraja la kwanza na shilingi 4,000 kutoka shilingi 3,000 kwa daraja la kati bei ambayo ndiyo inayotambulika.

Kissasi alisema zao la karafuu bado ni muhimili muhimu katika uchumi wa Zanzibar hivyo suala la kuachilia wakulima wakauze watakao linapaswa kuangaliwa kwa makini.

Alisema suala kuwaachilia huru wakulima wa zao hilo wakauze karafuu mahali popote serikali inalifanyiakazi na endapo itaona fursa hiyo ya kufanya hivyo haitosita kuchuakua hatua muafaka.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.