SERIKALI imewashauri wananchi waache kujenga karibu na kambi za jeshi la Ulinzi ili kuepuka athari za miripuko ya silaha zinazoweza kujitokeza za.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed alitoa ushauri huo barazani juzui.
Alisema wananchi ni vyema wafuate taratibu katika kujenga nyumba za makaazi na si vyema kuvamia maeneo ya kambi za jeshi.
Alifahamisha kuwa kambi za kijeshi zimekuwepo kabla ya kuwepo makaazi ya wananchi, hivyo ni jukumu la wanananchi kutokaribia kujenga pembezoni mwa kambi.
Alisema kuwa kambi za jeshi huwekwa kutokana na mahitaji ya ulinzi wa nchi na hivyo haziwezi kuhamishwa bali wananchi waache kuingia kwenye makambi hayo kwa kuchuakua maeneo ya ardhi na kujenga nyumba za kudumu katika maeneo ya jeshi.
Aidha katika hatua nyengine, Waziri huyo alisema hakuna sheria inayomruhusu askari yeyote kumpiga raia, ambapo askari anayefanya hivyo hatua za nidhamu hushukuliwa na wakuu wake.
Waziri Aboud alisema wananchi wanahaki ya kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria askari wanaowapiga.
Mwakilishi wa Micheweni, Subeit Khamis Faki, alisema baraza la Uchunguzi la Jeshi kwa kushirikiana na watalamu wa nchi rafiki zitazofanya chunguzi ya kuangalia usalama wa mabomu na silaha zinaweza kuharibu hali ya ulinzi kutokana kuingizwa ndani ya kambi za jeshi wataalum wa nje.
Waziri huyo alisema nchi rafiki zinazoshiriki kwenye uchunguzi huo ni zile zinazoaminika na hakuna shaka kama zinaweza kutoa siri za masuala ya ulinzi.
“Hawa ni watu tunaowaamini, ndio wanaotuuzia silaha, hakuna mambo ya kuuficha ulimwengu wa sasa ni wanasetlite wanatuona kila tunachofanya kuna siri gani inayofichwa kwenye dunia hii, alisema waziri huyo.
No comments:
Post a Comment