WAZIRI wa Kilimo na Maliasili, Mansoor Yussuf Himid amesema komba asili yake ni Mji Mkongwe wa Zanzibar tokea enzi na enzi za mabibi na mababu.
Kauli hiyo alitoa jana katika Baraza la Wawakilishi, kufuatia suala la nyongeza lililoulizwa na Mwakilishi wa Mji Mkongwe Ismail Jussa Ladhu aliyesema kwamba mji mkongwe wanaonekana jambo ambalo linaweza kuharibu harufu nzuri na mandhari ya mji huo kutokana na wanyama hao kuwa na harufu mbaya.
Waziri Mansour alisema kombo katika mji huo ndio asili yao, ambapo yeye aliwakuta na Jussa pia, ambapo alisisitiza harufu ya wanyama hao watu wameshaizoea.
Aidha akijibu swali la nyongeza la Mwakilishi Mwanajuma Faki Mdachi (Wanawake), aliyetaka ufafanuzi kwamba rasilimali za nchi zilizopo zinapotea, jambo ambalo linaweza kupoteza mapato ya taifa, aliekleza kwamba, baadhi ya rasilimali zinapotea nchini kutokana na ukataji wa misitu ovyo, hali iliyosababisha chui wa Zanzibar kupotea.
Mapema akijibu swali la msingi la Mwakilishi Mwanajuma juu ya athari kubwa za ukataji wa misitu iliyopo Zanzibar ni pamoja na kupoteza makaazi ya wanyama kama vile komba na kusababisha kukiombilia katika majumba makubwa yaliyopo maeneo mbali mbali kama vile Vuga, Mkunazini.
AWaziri huyo alifahamisha kuwa, maisha ya kombo kitabia ni tegemezi kwa binaadamu, hivyo ukweli huo unadhihirisha katika maeneo ya misitu mikubwa kama Jozani ambapo wanyama hao hutoka msituni nyakati za usiku na kuingia katika makaazi ya watu kwa ajili ya kutafuta chakula, ambapo hali hiyo inajitokeza katika Mji Mkongwe.
Alisema hatua zinazochukuliwa kudhibiti ukstsji wa miti ovyo na isiyo na lazima katika maeneo ya mijini, sio tu kwa kudhibiti upotevu wa wanyamapori, lakini pia kuimarisha hali ya mazingira na mandhari ya miji.
Hata hivyo alisisitiza kwam ba kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi wa misitu na wanyapori na umuhimu wake kwa jamii hapa nchini, sambamba na kuwashajihisha wananchi kupanda miti katika maeneo husika.
No comments:
Post a Comment