Habari za Punde

DK SHEIN AZURU WILAYA YA KUSINI LEO

 RAIS wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein , akifuatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Mwinyihaji Makame,baada ya kutembelea na kuona maendeleo ya ujenzi wa Tangi la Maji la,jimbo la Makunduchi, huko Kizimkazi Mkunguni jana, akiwa katika ziara wilaya ya kusini Unguja.


 Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wazee wa Makunduchi,Mkoa wa Kusini Unguja, akiwa katika ziara wilaya ya kusini na kuweka jiwe la Msingi soko katika kijiji hicho.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Moh'd Saleh Jidawi, alipotembelea Hopitali ya Mkoa huko Makunduchi jana, alipokuwa katika ziara ya wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja, kuangalia maendeleo katika sekta mbali mbali na kupata matatizo ya Wananchi.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwaangalia wagonjwa katika Hospitali ya Kotej Makunduchi, akiwa katika ziara ya wilaya ya Kusini , Mkoa wa Kusini Unguja leo.


Picha na Ramadhan Othman, Ikulu

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.