Habari za Punde

IBRAHIM MZEE ATEULIWA KATIBU WA BARAZA LA WAWAKILISHI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dk. Ali Mohammed Shein amemteua Ibrahim Mzee Ibrahim(45) kuwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Taarifa ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee imesema uteuzi huo umeanza tangu Mei 4, 2011.

Kabla ya uteuzi huo, Ibrahim Mzee alikuwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi ambaye aliteuliwa kwa mara ya kwanza mwaka Januari mwaka 2007 baada ya kustaafu kazi kwa Katibu wa Baraza hilo, Khamis Juma Chande.

Kitaaluma, Katibu Mzee ni mwanasheria mwenye Shahada ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kwa muda mrefu Katibu huyo alikuwa Afisa Mwandamizi katika Ofisi za Baraza la Wawakilishi.

Wakati huo huo, Rais Dk Ali Mohammed Shein, amemteua Abdulwakil Haji Hafidh kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Watu wenye Ulemavu Zanzibar. Mwenyekiti huyo pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar(ZSSF)

Rais amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa kifungu Na.9 ya sheria ya mwaka 2006. Uteuzi huo umeanza tangu Aprili 23, 2011.

IMETOLEWA NA:-
IDARA YA HABARI(MAELEZO) ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.