Habari za Punde

JUKUMU LA SERIKALI NI KUWATUMIKIA WANANCHI WOTE - DK SHEIN

Na Rajab Mkasaba, Pemba

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa jukumu lake kubwa ni kuwatumikia wananchi wote wa Unguja na Pemba bila ya ubaguzi.


Dk. Shein aliyasema hayo mara baada ya kulikagua bonde la mpunga la Mziwanda ambalo limeathirika na maji ya bahari kutokana na uharibifu wa mazingira ukiwemo ukataji wa mikoko ambayo ilkuwa inazuwia maji hayo ya bahari kuingia katika bonde hilo.

Akizungumza na wakulima wa bonde hilo, Dk. Shein aliwaeleza kuwa kilimo cha kijembe kongoroka mpini haina nafasi hivi sasa na lengo kubwa la serikali ni kuwasaidia wakulima wote wakiwemo wakulima wa muhogo, viazi, mikarafuu pamoja na wakulima wa mpunga kwa kuhakikisha wanapata mbegu bora, dawa, mabwana shamba pamoja na matekta na pembejeo nyenginezo.

Dk. Shein alitoa nafasi kwa viongozi aliofuatana nao wakiwemo Mawaziri husika kueleza lengo la serikali kupitia Wizara zao katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo ambao wote kwa walieleza mikakati liyowekwa ikiwemo kujenga ukuta wa zege paoja na kuutumia mradi wa TASAF 3.

Kwa upande wake Dk Shein alieleza kuwa hatua ya kwanza itakayochukuliwa ni kupeleka wataalamu katika bonde hilo ili wao watoe ushauri unaofaa ktika kutafuta njia za kulitatua tatizo hilo kwa mashirikiano ya Wizara kwa kuwatumia wataalamu wao.

Alisema kuwa ayo yatafanywa na serikali yenyewe na kuwasisitiz wananchi kutoharibu mazingira kwani athari zake ni kubwa sana.

Akiwa katika eneo lililotengwa kwa ajili ya maeneo huru ya vitega uchumi huko Michewei, Dk. Shein aliwaeleza wananchi wa Micheweni kuwa azma ya serikali anayoiongoza ni kuwapelekea maendeleo wananchi wa Micheweni na si vyenginevyo  na kusisitiza kuwa pato itakalopatkana ltawasaidia wao pamoja na wananchi wote wa Zanzibar.

Katika maelezo yake pia, Dk. Shein alisisitiza wazee wa Micheweni kwuasomesha watoto wao kwa bidii kwani kukamila kwa eneo hilo na kuanza kazi kutahitajia wafanyakazi ambao watakuwa na elimu, hivyo hawaa budi kuendeleza sekta hiyo.

Dk Shein pia, aliwafahamisha wananchi wa kijiji hicho juu ya Mfumo wa Serikali anayoingoza sanjari na njia zilizotumika katika kuwapata viongoi waliomo katika serikali hiyo.

Akiwa katika eneo la shamba la Mtama Mjini Wingwi, Dk. Shein alisisitiza kuwa serikali kupitia Wizara yake ya Kilimo na Wizara nyengine muhimu zitahakikisha zinatoa msaada mkubwa kwa wakulima hao wa mtama.

Dk. Shein alitembelea ujenzi wa barabara ya Wete-Konde yenye urefu wa kilomita 1.49 ambayo inajengwa na Kampuni ya MECCO ya hapa hapa nchini ambapo kwa maelezo ya Waziri wa Mawasiliao Hamad Masoud alisema kuwa ujenzi wa barabara hiyo uakamilika miezi kumi jayo.

Waziri huyo pia, aliwaeleza wananchi wa eneo hilo kuwa serikali imeamua kupunguza matumizi kwa kutengeneza njia ya mkato badala ya le ya mwanzo ili kupunguza gharama za ujenzi na kuwaahidi wananchi hao kuwa hata ile barabara ya mwanzo nayo itajengwa na kuwekwa lami hivyo wasione kwua wamedharauliwa.

Kwa upande wake Dk. Shein alisema kuwa lengo la serikali ni kuwatengenezea miundombinu wananchi zikiwemo baabara kwa madhumuni ya kuweza kusafirisha mazao, wagonjwa na kuwasaidia wananchi wenyewe katika shughuli zo za maendeleo. Alisema kuwa serikali imeamua kufanya hivyo ikiwa ni pamoja na kujiandaa na karne ya 21.

Dk. Shein pia, aliwaeleza wananchi na wananfunzi waliofika katika eneo la Pwale Gongo kuwa serikali imeamua kwa makususdi kuwasaidia wakulima wakiwemo wakulima wa mikarafuu pamoja na kuwasaidia wanafunzi kwa kuimarisha sekta ya elimu.

Pia, Dk. Shein litembelea ujenzi wa Tangi la juu la  kuhifadhia maji Gongoni ambapo mradi huo mara utakapomaliza utawasaiida kwa kiasi kikubwa wananchi wa Shehia za Kiuyu pamoja na Maziwangombe.

Aidha, Dk. Shein alielezwa kuwa serikali imo katika hatua za uchmbaji wa visima ambapo umalizika kwake vitaongea nguvu kwenye tangi hilo na kupelekea wananchi wote wa Micheweni kupata maji ya uhakika.

Dk. Shein pia, alifika eneo linalochimbwa matofali huko Kiuyu Mbuyuni na kujionea athari za uharibifu wa mazingira ambapo wachimbaji wa eneo hilo licha ya kuendelea kuchimba matofali hayo lakini wameonesha welew juu ya taratibu za uchimbaji ambapo mara wanapomaliza hufukia mashimo yao pamoja na kupanda mii ya kudumu na pia uchimbaji wao hauende chni sana.

Kutokana na hatua hiyo, Dk. Shein ameitak Wizara husika kuendelea kutoa elimu kwa wachimbaji wa Kangagani.

Pia, Dk. Shein alitemebele kituo cha redio jamii Micheweni na kuelezwa kuwa kituo hicho kimekuwa kikitoa elimu kwa wakaazi wa Michewni na vitongoji vyake juu ya elimu ya mazingira, kilimo, afya na mazingira, ufugaji na  uvuvi na kupongeza juhudi zinazochukuliwa.

Pamoja na hayo, Dk. Shein alipata nafasi ya kuzitembelea skuli mpya za Sekondari Wilaya ikiwemo skuli Sekondari ya Konde na Skuli ya Sekondari ya Chwaka ambazo zote kwa pamoja ujenzi wake unatarajiwa kukamilika mwezi wa Septemba ambapo Dk. Shein aliwasisitiza wanafunzi kujitahidi kusoma ili waje kuzitumia vyema skuli hio za kisasa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.