Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwasalimia wananchi na viongozi mbali mbali waliohudhuria katika sherehe za siku ya Mashujaa Tanzania,zilizofanyika jana huko katika makaburi na mnara maalum Naliendele Mtwara,(kushoto) Rais wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akitembelea makaburi ya Mashujaa yaliyopo Naliendele Mkoani Mtwara,katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa yaliyofanyika jana
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,(kulia) akiwa na Makamo wa Rais wa Tanzania Dk Moh'd Gharib Bilal,wakiwasalimia wazee waliopigania uhuru wa Tanzania katika sherehe za Mashujaa zilizofanyika huko katika viwanja vya Naliendele Mtwara jana
Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka silaha za jadi katika mnara wa kumbukumbu ya mashujaa wa vita vyaMsumbiji huko Naliendele, Mtwara katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa yaliyofanyika kitaifa Mkoani Mtwara jana
Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa majeshi nchini Bw Davis Mwamunyange.Picha na Ramadhan Othman, Mtwara
Bwana mpiga picha.
ReplyDeleteNaomba urekebishe kidogo hapo ulipoandika "wakiwasalimia wazee waliopigania uhuru wa Tanzania"
Lini Tanzania imepata uhuru? Huu sio ukweli na tusikubali kuipotosha historia. Mkoloni wa Tanzania alikuwa ni nani? Au Tanzania yenyewe ndio mkoloni.