Habari za Punde

MAZISHI YA MAREHEMU MUSSA KHAMIS SILIMA MWAKILISHI WA UZINI ZANZIBAR


Baadhi ya Wabunge pia walikuwepo kutoka kushoto ni Mhe Mrema, Mhe Zito Kabwe, Mhe Mbowe, Mhe Lowassa na Waziri Lukuvi

AFISA Itifaki wa Bunge Said Yakuob akitowa maelezo ya utaratibu wa mazishi.

WANANCHI wakihudhuria mazishi ya Mwakilishi wa Uzini na Mbunge kupitia Baraza la Wawakilishi Mussa Khamis Silima, yaliofanyika Kijiji kwao Kiboje Muembe Shauri. 

WANANCHI wakiwa katika viwanja vya Nyumba ya Marehemu katika kijiji cha Kiboje Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja. 

WAANDISHI wa habari wakifuatilia kwa karibu shughuli zote zamazishi ya marehemu Mussa Khamis Silima. 


SPIKA wa Bunge la Jamuhuri ya Tanzania Anna Makinda wa pili kushoto akiwa waMakamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania Mama  Asha Bilal, kulia Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Pili Balozi Seif na Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi nafasi za Wanawake Asha Bakari. wakiwa na wananchi wengi katika mazishi ya Mwakilishi wa Uzini kiboje.  

WANANCHI wakisubiri kuushindikiza Mwili wa Marehemu Mussa Khamis Silima katika makaburi yalioko kijiji kwao Kiboje.

WANANCHI wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu Mussa Khamis Silima , kwa ajili ya maziko yaliofanyika Kijiji kwao Kiboje Muembeshauri. 


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, kulia Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal,Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mustaf Ibrahim, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, kushoto Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho na Wananchi wakiusalia Mwili wa Marehemu Mussa Khamis Silima, katika sala inayoongozwa na Naibu Kadhi wa Zanzibar Khamis Haji Khamis.    

WABUNGE wa Bunge la Tanzania wakitowa salamu za pole kwa wafika walipowasili katika mazishi hayo huko katika Kijiji cha Kiboje kwa mazishi.

NAIBU Kadhi wa Zanzibar Khamis Haji Khamis akisoma duwa baada ya kumaliza kusalia maiti,Spika Pandu Ameir Kificho,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal,Mkuu wa Mkoa wa Kusini Mustafa Ibrahim, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad.    

WANANCHI wakiitikia duwa inayosomwa na Naibu Kadhi wa Zanzibar Khamis Haji Khamis baada ya kumaliza sala ya maiti. 



WANANCHI wakisoma hitma kabla ya sala ya maiti

WAHESHIMIWA Wabunge wakihudhuria mazishi ya Mbunge Mwenzao Mhe. Mussa Khamis Silima yaliofanyika kijiji kwao Kiboje Muembeshauri.

MAKAMU wa Rais wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Mhe Ali Mzee Ali alipowasili katika mazishi ya Marehemu Mussa Khamis Silima katika Kijiji cha Kiboje.

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal akiteta jambo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad, walipokuwa katika mazishi ya Mwakilishi wa Uzini Mussa Khamis Silima. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.