Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi
Jeshi la Polisi Kikosi cha Wanamaji Zanzibar kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama Babarini, limefanikiwa kukamata vipande 1,041 vya meno ya tembo yaliyokua akisafiirishwa kwa njia ya Bahari kwenda nchini Malaysia.
Afisa Uhusiano wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amesema kuwa vipande vya meno hayo vilikamatwa vikiwa ndani ya maguni 114 kati ya 135 yaliyokuwe kwenye konteina vikiwa vimechanganwa na dagaa wakavu kwenye magunia tayari kwa kusafirishwa kwa meli kwenda nje ya nchi kuuzwa.
Akizungumzia tukio hilo Bandarini hapo Mkuu wa Polisi Kikosi cha Wanamaji na Bandari mjini Zanzibar SP Martin Lisu, amesema kazi ya upekuzi wa magunia hayo kupata meno yaliyofichwa ilidumu kwa muda wa saa sita tangu ilipoanza majira ya saa 9.00 mchana jana hadi saa 3 usiku kwa kuvishirikisha vyombo vya Polisi, TRA, KMKM, Uhamiaji, Utasalama wa Taifa, Viongozi na Askari wa Mamlaka ya Bandari.
Aidha Viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar kamishna Mussa Ali Mussa, Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi Zanzibar ACP Muhudi Mshihiri, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini magharibi ACP Aziz Juma Mohamme na Mkuu wa Upelelezi wa mkoa huo ACP Ahmada Abdallah na Viongozi wa Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama.
Watuhumiwa wawili waliohusika na meno hayo akiwemo Msafirishaji Raman Msigalo na Ramadhan Pandu wa Mwanakwerekwe, wamekamatwa na walipelekwa katika kituo Kikuu cha Polisi cha Madema kwa mahojiano zaidi.
Katika Hatua nyingine, Makachero wa Polisi kutoka Makao Makuu wa Upelelezi Jijini Dar es Salaam na Polisi wa Kimataifa (Interpol) hapa nchini wakiongozwa na Kamishna Msaidi wa Polisi Hamisi Mkumbo, wamewasili mjini Zanzibar leo yatari kwa mahojiano ya kina na watuhumiwa.
Uzito na thamani kamili ya meno hayo bado kujulikana na kwamba Jeshi la Polisi linasugua vichwa kujua wapi meneo hayo yametoka na yamekusanywa kwa muga gani na akina nani.
Hiyo ni shehena ya kwanza kubwa kukamatwa kwa meno ya tembo visiwani humo tangu historia ya usafirishaji wa meno kama hayo kwenda nje ya nchi kwa njia ya bahari.
No comments:
Post a Comment