Habari za Punde

SERIKALI KUFUATILIA MWENENDO WA BIASHARA YA KARAFUU - BALOZI SEIF




Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya kushuhulikia Mashamba ya Serikali,  ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais Wa Zanzibar Mhe, Balozi Seif Ali Iddi akiwa na ujumbe wake walipotembelea kambi ya uchumaji wa zao la Karafuu ya Bw. Salum Mbaruku Salum iliyopo Kijiji Cha Ngwachani, Mkoa wa Kusini Pemba, Kamati nzima ya kushughulikia Mashamba ya Serikali ipo Kisiwani Pemba kwa ziara maalum.



Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe, Balozi Seif Ali Iddi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Maalum iliyoundwa kushughulikia Mashamba ya Serikali, akikagua Karafuu za mkulima Bw, Ali Salim Ali wa Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba aliyekutwa akizichambua tayari kwa mauzo katika Shirika la Taifa La Biashara la Zstc




Mwenyekiti wa Kamati ya kushughulikia Mashamba ya Serikali akikagua zao la Karafuu ambazo tayari zimeshanunuliwa na Shirika la Zstc zikiwa Ghala kuu la Mkoani.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kuziagiza Afisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo Mombasa Kenya ,Malaysia na India kufuatilia mwenendo wa biashara ya karafuu unaofanywa na baadhi ya Wafanyabiashara wa Kenya wanaoijihusisha na uuzaji wa Karafuu za Zanzibar Nje ya Nchi.


Uuzaji huo ambao unachangia kudhoofisha uchumi wa Zanzibar unafanywa kinyume na sheria za biashara za Kimataifa kwa vile zao hilo haioteshwi Nchini Kenya.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddiameeleza hayo wakati wa ziara ya yake ya siku tano kisiwani Pemba kuhamasisha uokoaji wa zao la Karafuu.

Balozi Seif akiwa Mwnyekiti wa Kamati maalum ya kushughulikia mashamba ya Serikali Kisiwani Pemba amesem kitendo cha baadhi ya Wafanyabiashara hao wa Kenya wanaojihusisha na baiashara ya karafuu ya Zanzibar hakina budi kukomeshwa kwa lengo la kunusuru upoteajikiholela wa zao hilo ambalo ni uti wa mgongo wa uchumi wa Zanzibar.

“ Hili agizo litazihusu Afisi zetu wa Ubalozi za Tanzania zilizopo India, Mombasa na Malaysia kupitia Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko Zanzibar kulinda Karafuu zetu” Alisema Balozi Seidf Ali Iddi.

Akizungumzia suala la usalama wa fedha za Wakulima na Wauzaji wa Karafuu Blaozi Seif ameiagiza Benki ya watu wa Zaznaibar { PBZ } kuangalia uwezekano wa kufungua Matawi yake katika vituo vya ununuzi vilivyopo Vijijini ili kulinda fedha za wakulima hao.

Balozi Seif amesema tabia ya baadhi ya watu waovu wanaweza kuitumia nafasi hiyo kutaka utajiri wa haraka kwa kutumia migongo ya wakulima hao ambapo tayari amesema dalili zimeanza kujichomoza.

Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amevitembelea vituo vya ununuzi wa Karafuu vya Ngwachani,Kangani pamoja na Maghala ya shirika la Taifa la Biashara ya bandarini Mkoani na Madungu Chake Chake.

Mapema Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Nd Jabu Khamis Mbwana amemueleza Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwamba jumla ya gunia 141 za Karafuu Kavu zimekamatwa hadi kufikia jumapili kufuatia msako mkali uliofanywa kati ya Maafisa wa Kamati ya Ulinzi, Wananchi, Mashepa kupitia mpango wa Polisi Jamii.

Karafuu hizo zinazokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni Mia Moja zilikuwa zimeshatayarishwa kwa nia ya kusafirishwa nje ya Nchi Kimagendo.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
6/9/2011.

1 comment:

  1. Hongereni sana Bw. Othman Ame na Brother Mapara kwa kuendelea kutuhabarisha yanayo tokea visiwani kln. bado nahitaji ufafanuzi kidogo.Hivi kumbe S.M.Z inamiliki mashamba ya mikarafuu? na kama ni hivyo ni mashamba mangapi na yana ukubwa gani? na kama kweli yapo basi itakuwa hata hayashughulikiwi! na kama kawaida yetu watu hawana hata interest ya kujua.Nakumbuka baba yangu aliwahi kunikhadithia kua baada ya mapinduzi S.M.Z Iligawa heka tatu kwa wengi wa wananchi wasiokua na ardhi kwa ajili ya kilimo lkn. cha kushangaza walio wengi wameyauza,kuyakata viwanya na hata kuyatelekeza na SMZ ktk kipindi chote hicho (zaidi ya miaka45) haijawahi kutoa tamko wala kutokea mzanzibari yeyote kuulizia hatma ya zile heka tatu tatu. si wabunge wala wawakilishi..Jamani panasomwa nini? nadhani hata hizo nyaraka zinazoonyesha ipi alipewa nani,hazipo tena! serekali ilitakiwa angalau iwashauri tu wale walioamua kukata viwanja heka zao kua wakate kwa plani..ah wapi? watoto wetu watakuja kujiuliza kama kweli tulikua na akili timamu!" MAENEO YENYE RUTBA YANAJENGWA HALAFU YA UWANDA NDIO YANAPANDWA MITI"...Ndugu zangu naulizwa tena "panasomwa nini?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.