Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameagiza kuvunjwa kwa vibanda vya kudumu vya biashara vilivyojengwa pembezoni mwa soko la Wavuvi liliopo Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Balozi Seif ametoa agizo hilo baada ya kufanya ziara ya ghafla katika eneo hilo na kuona Vibanda hivyo ambavyo ujenzi wake haukuzingatia Sheria.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewataka watu waliojenga katika eneo hilo kuhakikisha wanavunja majengo yao kwa vile yanaharibu haiba ya eneo hilo.
Amesema Sehemu hiyo imetengwa maalum kwa wavuvi kuuza samaki wao kupitia soko lililojengwa na Halmashauri ya Wilaya ya Magharibi.
“ Hivi Vibanda mbali ya kuchafua haiba ya Soko hili lakini pia vinasababisha kukosekana na usalama wa Viongozi na inatokana na baadhi ya Vibanda hivyo kujengwa ndani ya eneo la ukuta wa Majengo hayo ya Viongozi ”. Alisema Balozi Seif.
Balozi Seif ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Magharibi kulifanyia matengenezo Jengo la Soko hiyo ambayo haliko katika hali ya kuridhisha.
Amesema haipendezi kuona Jengo hilo linalalamikiwa na Wavuvi kutokana na uchakavu wake wakati Mapato yanaendelea kukusanywa kila siku.
Balozi Seif ametahadharisha kwamba atafanya ziara katika kipindi kifupi kijacho kuangalia iwapo agizo hilo limetekelezwa vyenginevyo taratibu za kisheria zitatekelezwa.
Eneo la fukwe ya mazizini ambalo limekuwa likutumika kwa shughuli za wavuvi wadago kwa muda mrefu hivi sasa linaonekana kuwa na shughuli za makaazi ya kudumu.
HONGERA MZEE!
ReplyDelete