Habari za Punde

WIZARA YAPEMBUA MKANDARASI BARABARA YA JENDELE - UNGUJA UKUU

Nafisa Madai, Maelezo

WAZIRI wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar, Hamad Masoud Hamad amesema timu ya wataalamu wa wizara wanaendelea na utaratibu wa kumtafuta mkandarasi mwenye sifa na viwango bora vya ujenzi wa barabara ya Jendele- Unguja Ukuu.

Waziri Massoud alieleza hayo alipokuwa akizungumza na wananchi na wakulima wa kijiji cha Cheju walipotaka kujua ujenzi wa barabara hiyo matayarisho yake yamefikia wapi.


Aidha alisema ujenzi wa barabara hiyo unategemea kuanza mwanzoni mwa mwaka ujao ambapo ujenzi wake utazikutanisha barabara ya Jendele-Cheju na kunganishwa hadi Unguja Ukuu Kaebona.

Barabara hizo alisema zitajengwa kwa kiwango cha lami kwa mkopo nafuu kutoka benki ya maendeleo ya kiarabu kwa nchi za Afrika BADEA, ikishirikiana na serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Waziri huyo alisema katika kutekeleza ahadi na maamuzi ya serikali kwa wananchi wake hakuna budi miundimbinu hiyo ya barabara kufikia kila sehemu ya mahitaji ya wanachi kwa lengo la kuwarahisishia usafiri kupitia barabara.

Hata hivyo alisema hadi sasa wakandarasi watano wamejitokeza kutaka kupewa fursa ya kujenga barabara hiyo ambapo alisema yeye mwenyewe akishirikiana na wataalamu wake wanakaa pamoja kujadili maombi ya wakandarasi hao na kutoa matokea ya kumtangaza mkandarasi aliyebora na atakaweza kujenga kulingana na hali ya kifedha iliyopo.

Wakati huo huo waziri Massoud alifanya ziara ya hafla ya kukagua ujenzi wa daraja la Mwera unaoendelea hivi sasa ambapo alishuhudi utiaji zege na kuitaka kampuni inayojenga daraja hilo kukabidhi rasmi daraja hilo katika mikono ya serikali si zaidi ya Disemba 31 mwaka huu.

Aidha alisema imani yake kubwa kuchelewa kwa ujenzi huo kampuni hiyo itajenga daraja hilo kwa ubora wa hali ya juu na kuweza kutumika bila ya hofu kwa gari ambazo zitabeba mizigo mikubwa.

Sambamba na hayo waziri Hamad aliwataka wananchi wa Mwera kuwa wastahamilivu katika kipindi chote cha matengenezo na kuwaomba watoe mashirikiano makubwa kwa kampuni hiyo ili ujenzi huo uweze kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Kwa upande wake Injiania Mkuu wa ujenzi huo, Chales Mwangande alisema ujenzi huo ulitegemea kumalizika Septemba mwaka huu lakini kutoka na sababu mbalimbali zikiwemo hali ya hewa (mvua) ndiko kuliko walazimu kuchelewesha ujenzi huo.

Injinia huyo alimuhakikishia waziri huyo kuwa ikfikapo Disemba 31 kazi hiyo itakuwa imekamilika rasmi na kuweza kutoa fursa kwa watumiaji wa barabara hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.