ANAHITAJI SHILINGI MILIONI MOJA NA NUSU ILI KUPATA TIBA YA MGUU WAKE.
KIJANA Henry Nazaremo Sanga, (30), Mkaazi wa Amani Magogoni Mjini Unguja, anaomba kupatiwa msaada wa matibabu ya mguu baada ya kuumia akiwa kazini.
Kijana huyo ambaye alifika katika 0fisi za gazeti hili Rahaleo juzi ameomba kupatiwa msaada huo baada ya kuambiwa zinahitajika shilingi Milioni 1.5.
Henry amesema tangu apate ajali hiyo ni mwaka mmoja na nusu sasa. Alisema alihitaji kufanyiwa upasuaji tokea wakati huo katika hospitali ya Bukele, Mkoa wa Pwani lakini ameshindwa kutokana na gharama.
Alisema hivi sasa amekuwa akipata tabu kuendesha maisha yake kutokana na maumivu yanayompata kutoka katika mguu huo, hali inayomfanya ashindwe kujiendesha kimaisha.
Katika hatua nyengine, Henry alisema baadhi ya watu waliokuwa wakimpatia mahitaji ya chakula wameanza kumchoka hali inayozidisha usumbufu zaidi.
Alisema tatizo la mguu huo ulitokana na kuumia wakati akijaribu kuzamia baharini kwani ndio shughuli zake alizokuwa akizifanya kwa muda mrefu, lakini kwa bahati mbaya aliumia na kusababishwa kulazwa hospitali
kwa kipindi kirefu kutokana na damu kuganda baada ya kufungwa P.O.P.
Alisisitiza kwamba anachohitaji kupata fedha hizo kwa vile tayari ameshafanyiwa uchunguzi na kuahidiwa anaweza kupata nafuu ikiwa atafanya matibabu hayo.
Kijana huyo alifahamisha ili aweze kupokea misaada hiyo anawaomba wananchi kumsaidia kwa kumtafuta kwa nambari za simu 0773285020.
UNAWEZA KUWASILIANA NAE KWA NAMBA YA SIMU 0773285020
pole sana kaka Henry!..lkn naona hukutoa no. za account. kumbuka sio watu wote watu wote wanaosoma mtandao huu kua wapo z'bar. na wala sio wote wenye uwezo wa kukusaidia 1.5ml. wengine uwezo wao ni 5000 au 10,000 nk. lakini zaidi ni hii no. ya simu, hakuna mbadala? watu wengine "watata" akiona z'tel yeye ana voda, tigo au airtell anaona ..ohoo!
ReplyDelete