Tunapenda kutoa tarifa hii ya kwamba Mtajwa hapo juu ni kijana ambae wengi wetu tunamfahamu kutokana na kushiriki kwake katika tafrija mbali mbali ambazo zimekua zikiandaliwa kwenye vitongoji mbali mbali vya mji wa Washington Seattle.
AbdulKarim, kama anavyojuulikana kwa umaarufu ''DOCTOR'', ameshikiliwa na Idara ya Uhamiaji katika jela la Tacoma kwa takribani miezi sita sasa.
Taarifa rasmi zinazopatikana kutoka kwa Mwanasheria wake ni kamba ''Doctor'' anakabiliwa na kesi ya Uhamiaji. Kesi ya kijana huyu imeshasoma mara kadhaa na kutokana na kazi nzuri za Kisheria anazozifanya Wakili wake ''Doctor'' amefanikiwa kupewa Dhamana ya kuwepo nje huku kesi yake ikiwa inaendelea kwenye vyombo vya sheria.
Juhudi mbali mbali zilifanywa ili kuweza kuwakusanya marafiki wanaomfahamu ili kuweza kumsaidia kwa kumpatia michango a kifedha kwa nia safi ya kuweza kumsaidia ili aweze kuwepo nje ya jela, ili iwe ni pamoja na kupata wakati muafaka wa kuwasiliana na kufuatilia kesi inayomkabili.
Naomba kueleza kwa ufupi juhudi kadhaa ambazo zilifanywa kuanzia mwanzoni chini ya Usimamizi wa Dada Flora Komba, juhudi ambazo ziliwezesha kupatikana mchango wa kuweza kumpatia Wakili wa kusimamia kesi yake. Flora aliendelea kuwa ni muhimili wa kusaidia mawazo na mipango mbali mbali, lakini kwa bahati mbaya Mwenyezi Mungu amempa mtihani wa kuumwa.
Naomba Mwenyezi Mungu amuondolee maradhi hayo ili aweze kurudi katika afya njema (Ameen). Mchango mwengine uliitishwa na kuweza kupatikana idadi ya Dola za Kimarekani takriban 1200. Pamoja na ahadi kadhaa za kuchangia ambapo wengi wetu hatukuweza kukamilisha ahadi hizi kutokana na matatizo yanayotukabili katika wakati huu mgumu.
''Doctor'' amepewa dhamana ya kuwepo nje kwa kulipwa fedha taslimu Dola za Kimarekani 12,000. Juhudi mbali mbali zilifanywa ili kuweza kumpatia dhamani hiyo kutoka kwenye makampuni yanayoshughulikia masuala ya dhamana kwa kulipa asilimia fulani, lakini kwa bahati mbaya vipengele vilivyowekwa katika upatikanaji wa dhamana hiyo vilikua ni vigumu kuweza kutekelezeka.
Mara kwa mara ninapopata fursa ya kuwasiliana na Doctor akiwa jela amekua akinitaka niwasilishe ujumbe huu kwenu ili tuweze kumsaidia kumpatia kiwango hicho cha pesa ili aweze kuwepo nje ya jela, hii ni kutokana na ugumu wa maisha anayo pambana nayo, pamoja na kwamba anasumbuliwa na maradhi na Kisukari(Diabetic) na hali halisi ya jela.
Bila shaka kiwango cha pesa kinachohitajika kwa ajili ya dhamana yake ni kikubwa. Bali nimeonelea ni vyema nitume ujumbe huu kwenu ili tuweze kutafakari upya ni namna gani tunaweza kuungana katika kumpatia msaada. Vikao kadhaa vya jinsi ya kumsaidia vilizaa malumbano makali na hatimae tukapoteza muelekeo wa kufanikisha lengo hili. Lakini muhusika amekua akiomba msaada kwa majonzi na vilio hali ambao imenipelekea nililete tena suala hili kwenu.
Tulipokutana kwa mara ya mwisho katika kulifikiria suala hili tulikuja na wazo la kuweza kujikusanya miongoni mwetu na kupata watu angalau 60, ili kuweza kuchangia Dola; Mia mbili kwa kila mmoja wetu. $200X60=$12000. Naomba mupokee ombi hili ili tuweze kufanikisha msaada huu kwa kijana huyu, ambae anaendelea kusononeka kwa huzuni huku akipambana na maisha magumu ya jela.
Kesi yake ilisomwa kwa mara ya mwisho Tarehe 26. 10. 2011 na dhamana yake bado iko wazi hadi kesi yake itakaposomwa tena tarehe 29.11.2011.
Kwa wale wote ambao wako tayari kuweza kutoa msaada kwa Bwana AbduliKarim (Doctor) wanaweza kuwasiliana na wafuatao:
1. Muta
2. Abdullah Machano (Dulla 2g)
3. Haji Rajab Haji
4. Masoud Kayanda
5. Mohamed Ngwali
Au Mtu yoyote ambae anakubaliana na wazo hili anaweza kuwasilisha mchango huo kwa waliotajwa hapo juu pia.
Nia na madhumuni ni kufanikisha mchango huu ndani ya kipindi cha wiki 2, ingawa kwa wale ambao wataweza kufanikisha kabla ya tarehe ya kesi yake hapo October 29, 2011 pia wanaweza kuwasiliana nasi.
Natanguliza samahani iwapo taarifa hii italeta usumbuvu wa aina moja au nyengine. Iwapo kuna mawazo yoyote juu ya suala hili naomba tuwasiliane. Nia na madhumuni ya mchango huu si kuvunja taratibu za Serikali kwa njia ya aina yoyote ile katika kufuatilia kesi yake, bali ni kuweza kushirikiana kutokana na kujuana na kufahamiana kwetu.
Wenu Rafiki,
Haji Rajab Haji.
No comments:
Post a Comment