Chuo Kikuu cha Indiana (Indiana University-USA) kinahitaji mwanafunzi ambae ataweza kusoma PhD au Masters ya Linguistics, Second Language Studies au TESOL.
Mwanafunzi atakuwa pia anafundisha Kiswahili kuanzia Fall 2012(September). Mwanafunzi huyo atalipiwa masomo yake na chuo na pia atalipwa pesa za kujikimu. Ni vizuri kama mwanafunzi huyo atakuwa na uzoefu wa kufundisha Kiswahili kwa wageni.
Utaratibu wa kuomba ni kuwa mwanafunzi huyo inabidi aombe masomo hayo kwanza (Kusoma Linguistics au Second Language Studies au TESOL. Mara atakapokubaliwa kusoma, awasiliane na Dr Alwiya Omar kwa email aomar@indiana.edu au Abdulwahid Mazrui kwa email ammazrui@umail.iu.edu.
Mwisho wa kupokea maombi ya masomo ni December 31, 2011.
Kumbuka ni lazima kuomba masomo kwanza. Kujua zaidi kuhusu maombi ya masomo ingia hapa:
Ili upate nafasi ya kusoma Marekani unahitaji kufanya mtihani wa GRE:
Pia ufanye mtihani wa TOEFL
Kama mtu atahitaji msaada kuhusiana na maombi hayo, basi awasiliane na Abdulwahid Mazrui.ammazrui@umail.iu.edu
No comments:
Post a Comment