Marais wastaafu wa Zanzibar wa awamu ya tano na sita Dk Salmin Amour Juma na Dk Aman Abeid Karume wanatarajiwa kutunukiwa Shahada ya heshma ya Udaktari katika mahafali ya Saba ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Chuo hicho imeeleza kwamba Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein atawatunuku Viongozi hao katika Mahfali hayo.
Mahafali hayo yanatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Chuo hicho Vuga mjini Zanzibar Jumamosi ya wiki hii.
Aidha Dk.Shein atawatunuku vyeti katika ngazi mbali mbali za Stashada na Shahada kwa wahitimu wa mwaka 2010/2011 wa fani mbali mbali.
Kufanyika kwa Mahfali hayo ya saba kunaenda samba mba na maadhimisho ya miaka kumi ya Chuo hicho tangu kuazishwa kwake mwaka 2003.
Kabla ya Mahfali hayo shughuli mbalimbali zilifanyika ikiwa ni sehemu ya shamra shamra ya kufikia miaka 10 tangu kuanzishwa Chuo hicho
Miongoni mwa shughuli hizo ni pamoja na Kongamano lililozungumzia athari ya mabadiliko ya hali ya hewa ambayo inaathiri visiwa vidogo vidogo Duniani.
Aidha kulifanyika maonesho ya kazi mbali mbali zinazofanywa na Chuo hicho katika jitihada zake za kunyanyua taaluma.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR 22/12/2011
No comments:
Post a Comment