ZAIDI ya watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi mwishoni mwa wiki iliopita walivamia hoteli ya Dongwe Anna of Zanzibar ilioko Bwejuu na kukimbia na kasha lenye mamilioni ya shilingi
Kamanda wa polisi Mkoa wa Kusini Unguja ACP Agustino Olomi ameliambia gazeti hili kwamba majambazi hao walifanikiwa kuondoka na kasha lililokuwa na dola za Marekani, 4000, Euro 3500 na fedha taslim shilingi 2,000,000 pamoja na kumputa ndogo (laptop mbili).
Hata hivyo, Kamanda Olomi alisema majambazi hao walipojaribu kulivunja kasha hilo hawakufanikiwa, ndipo polisi waliokuwa wakimbizana na majambazi hao walifanikiwa kuzipata fedha hizo katika fukwe za hoteli hiyo.
Hata hivyo, Kamanda Olomi alisema hakuna mtu aliejeruhiwa katika tukio hilo na majambazi waliohusika walikimbia bila kufahamika.
Wakati huo huo, Kamanda Olomi amethibitisha kutokea tukio jengine ambapo mlinzi wa ofisi ya halmashauri ya wilaya ya kusini, Idi Hassan Ameir wa Kitogani amejeruhiwa sehemu ya kichwani na mkononi na watu wasiojulikana ambapo inaaminika huenda ni majambazi waliohusika na wizi kwenye hoteli hiyo ya Dongwe.
Kamanda Olomi alithibitisha kufanyika kwa matukio yote mawili na kusema watu wawili walikuwa wakilinda ofisi hiyo lakini mmoja hawakufanikiwa kumpata.
Alimtaja mlinzi mwenzake kuwa ni Ali Haji Ussi aliewatoroka majambazi hao na kwenda kijijini kuomba msaada wa wananchi.
Kamanda huyo alisema kuwa majambazi hao hawakufanikiwa kuondoka na kitu chochote katika ofisi hiyo na hali ya kijana huyo ilikuwa ikiendelea vizuri baada ya kulazwa na kuruhusiwa siku iliofuata.
Hivyo hivyo, Kamanda Olomi ametoa wito kwa wamiliki wa hoteli katika Mkoa wa Kusini kutoweka fedha nyingi katika hoteli zao na kutaka kuomba msaada wa polisi wanapohamisha fedha au wanapokwenda Benki kuchukua fedha.
hao majambazi wanatokana na serikali ya zanzibar kuondosha passport watu kutoka tanzania bara wanaingia zanzibar kama wanakwenda temeke kwa haya mambo yote serikali ndio responsible.
ReplyDeleteAcha hizo,ujambazi hauna kwao!..wangewezaje bila ushirikiano na wenyeji?
ReplyDelete